Dar es Salaam
Ameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kutumia Kitengo cha Mkaguzi wa ndani na Kufanya Ukaguzi wa mara kwa mara.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam *Mhe Albert Chalamila akiwa katika kikao cha Baraza maalum la kupitia hoja za mdhibiti na mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) katika Manispaa ya Kigamboni ameitaka Halmashauri hiyo kuwa na mikakati ya kuzuia hoja za CAG zisiwepo kabisa.
RC Chalamila ameipongeza Manispaa ya Kigamboni kwa kupata hati safi katika Kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 kufuatia ripoti ya CAG kufanikiwa katika ukusanyaji wa mapato ambapo mpaka sasa kuelekea kuisha kwa mwaka wa fedha Manispaa imefikia asilimia 114 ya ukusanyaji na kwa jinsi wanavyofanya juhudi kujibu hoja kwa wakati.
Aidha kwa muktadha huo RC Chalamila ameelekeza juhudi kubwa iwekwe katika kuzuia hoja zisitokee na sio kujipanga kujibu, hivyo amewataka kuhakikisha zoezi la ukaguzi linakuwa endelevu, vilevile kila Halmashauri ijengee uwezo kitengo cha mkaguzi na kukifanya kuwa ni jicho lake na kukitumia vizuri.
Aidha RC Chalamila amewataka kujibu kwa wakati hoja za CAG, Utekelezaji wa maagizo ya LAAC, kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wanaoisababishia Halmashauri hoja*, na kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato na kudhibiti upotevu wa fedha za umma.
Sambamba na hilo amelitaka Baraza la Madiwani kutekeleza wajibu wake'' kwa kuisimamia vyema Manispaa. @kigambonimanispaa @halima_bulembo



0 Comments