MKUTANO WA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA UTAFUNGULIWA 9 DISEMBA NA RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSANI JIJINI DARE ES ALAM


Na:  Sheila  Ahmadi. 


Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassani  atafungua mkutano wa kwanza wa kitaifa wa dira ya maendeleo ya taifa  utakaofanyika jijini Dar  es Salaam Disemba 9 lengo la mkutano huo ni kupokea na kujadili taarifa za tathmini  ya utekelezaji wa dira hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari  Jijini  Dar es Salaam Waziri wa Nchi, OFisi  ya  Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa  Kitila  Mkumbo amesema taarifa hiyo ya kitafiti inaenda kutekeleza  dira ya taifa ya maendeleo mwaka 2025, huku mambo mengine yakitekelezwa na kuonesha kuwa pato la Mtanzania limeongezeka kutoka dola za kimarekani 1,200 kwa mwaka 2022.





Aidha waziri  Kitila amesema Tanzania  imefikia asilimia 124  ya kujitolea kwa chakula huku ikilinganishwa  na lengo la kufikia asilimia 140 ifikapo mwaka 2025  hatua hiyo imewezesha Tanzania  kukabiliana na njaa kwa mikoa na wilaya zote nchini .

"Mtandao  wa barabara za lami  na zege (Paved Roads ) katika mikoa umeongezeka kutoka Kilomita 4 , 179  mwaka 2000 hadi kufikia kilomita 11, 966.8 kwa mwaka 2023  na mafanikio mengine ni pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 760  kwa vizazi hai  100, 000 mwaka 2000 hadi kufikia vifo  104  na mwaka 2022  ikiwa tumevuka lengo  la kufikia vifo 265 ifikapo mwaka 2025.

Kutokana na mkutano huo  Rai  samia atazindua rasmi timu  kuu ya kitaalamu  ya dira  (National vission core  Technical  Team  na kamati ya usimamizi  wa dira   (Natonal  vission steering  comitee)  pamoja na nyenzo  Za kidigitali ambazo zitaenda  kutumika katika kkusanya  maoni ya wadau.

Hata hivyo  amesema kutokana na zoezi la kuandaa dira mpya ya maendeleo  iwe jumuishi na shirikishi  ambapo mkutano huo utahudhuriwa na wadau mbalimbali  kutoka pande zote za nchi wadau hao wakiwemo  viongozi wakuu wa serikali  ya tanzania serikali kutoka Zanzibar, Mawaziri, makatibu wakuu, na wakuu wa mikoa  na Taasisi nyingine binafsi.

Ametoa  wito  kwa wananchi  kuweza  kufatilia mchakato wa kuandaa dira hiyo  mpya na kushiriki kikamilifu katika kutoa  maoni  yao kuhusu Tanzania waitakayo  katika miaka ijayo.

Post a Comment

0 Comments