Na Sheila Ahmadi
Akizungumza katika uzinduzi huo mkurugenzi mtendaji kutoka shirika lisilo la kiserikali Liberty sparks Evans Exaud amesema kuwa kutokana na kilimo hicho baadhi ya wananchi waishio katika vijiji hutumia kilimo kama kipato hivyo huwapelekea wengi wao kutatua changamoto zao mbalimbali ambazo ni mali pekee ya thamani na kudumu .
Mchango wa wanawake waishio vijijini ni mkubwa haupaswi kuupuzwa hata kidogo kwani maendeleo ya kiuchumi tanzania hutokana na kilimo katika kufikia uchumi wa kati nchini na imekua kimbilio kubwa kwa wakulima hivyo sekta ya kilimo mifugo, uvuvi, vinachangia asilimia 26.9 ya pato la taifa kwa mwaka uliopita ambapo kulikuwa na kiwango cha uchangiaji na ukuaji wa mapato la taifa ulikuwa mifugo7.1% misitu 2.7% uvuvi 1.7% na Mazao 15.4%.
Kutokana na migogoro kuwa miji vijijini na wanawake waathirika ni wengi ambayo inatokana na ardhi imeenda kutokea kwenye mabaraza na mahakama za mijini hususani kwenye maeneo ambayo hayajapimwa na kuhakiki huku wadau wa ardhi wakichambua kwa kina matatizo yanayohusiana na ardhi na kushauri maboresho yatakayomaliza matatizo na kupunguza migogoro ya ardhi nchini Tanzania. " Amesema mkurugenzi Evance"
"Serikali imeendelea kupitia utaratibu wa umilikishwaji wa ardhi na garama zake ili kuweza kuwezesha wantanzania wote hususani Masikini ambao wanaishi kijijini na kumiliki ardhi kihalali huku vikwazo vyote vitokanavyo na zoezi zima la upimaji wa ardhi vijijini na kupunguza mlolongo mrefu wa upatikanaji wake wa kitaaalaam inayohitaji mtaji wa mkubwa na urahisishaji wake na kugubikwa na changamoto nyingi.
Kwa upande wake Mdau ambae ameshiriki katika mkutano huo Elias nawera ameipongeza shirika hilo kwa kuweza kushiriki katika uzinduzi huo ambao umeenda kupelekea chachu kwa wakulima wa ardhi na wananchi waioshio vijijini ambao ardhi kwao ni ajira hivyo hujikwamua katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi katika kukuza nchi



0 Comments