ZOEZI LA KUHAMISHA WANANCHI WA NGORONGORO AWAMU YA PILI LANUKIA





Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Mobhare Matinyi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema kwamba Awamu ya Pili ya kuwahamisha wananchi wa Ngorongoro kwa hiari yao na kuwapeleka katika maeneo yaliyotengwa likiwemo la Msomera Wilayani Handeni mkoani Tanga imeanza Julai mwaka huu na inatarajiwa kukamilika Machi 2024.

Hayo yamebainishwa leo Desemba 3, na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kuwahamisha wananchi wa Ngorongoro.

Matinyi ameeleza kuwa katika Awamu ya Kanza Msomera kulijengwa nyumba 503, na kuwezesha Kaya 551 kuhamia zikiwa na jumla ya watu 3010 na mifugo 2521.

"Katika eneo hili na Msomera, ili wananchi wahamie kwa hiari Sirikali ilifanya mambo mawaili. Moja ilitoa elimu kwa wananchi, kwanini imefika wakati wa kuwahamisha Ngorongoro na kuwapeleka kwenye maeneo waliyowatengea. Na jambo lingine la msingi sana ni Serikali kuhakikisha kuwa inalinda haki za watu hawa na kuwapa vitu vitakavyowashawishi na kuwasaidia katika maeneo hayo," amesema Matinyi na kuongeza, 

"Vifuatao vikapangwa na kutekelezwa, kwa kila Kaya inayokwenda Msomera inajengewa na kupewa nyumba bure nyenye vyumba vitatu vya kulala. Nymba hiyo inakaa kwenye eneo la eka mbili na nusu na anayehamia hapo anapewa hati miliki ya eneo lake. Mwananchi huyo pia anapewa eneo la ekari tano likiwa na hati miliki, iwapo anamifugo kuna eneo ambalo Serikali imelitenga kwa ajili ya malisho ya mifugo,".

Serikali haikuishia hapo tu, Matinyi amebainisha kuwa Serikali ilaamua kujenga mabwawa kwa ajili ya maji ya mifugo na kuchimba visima kwa ajili ya maji ya watu hao na kuweka miundombinu ya kuyasambaza ili kuwafikiwa wananchi.

"Serikali pia ikasema inapomuondoa mtu ngorongoro, inamlipa fidia kwa ajili ya majengo yake. Serikali inafanya tathimini ya kila kitu kilichopo pale na inamlipa fidia. Unapewa fidia na shilingi milioni 10, halafu Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inakuhamisha wewe na familia yako, vitu vyako na mifugo kama unayo kutoka Ngorongoro mpaka Msomera bila kutozwa chochote," amebainishwa Msemaji Mkuu wa Serikali Matinyi.

Hivyo ameeleza kuwa katika awamu ya kwanza kazi kubwa ilifanywa, hivyo na katika awamu hii ya pili iliyoanza Julai mwaka, lengo ni kujenga nyumba 5000 katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wananchi wa Ngorongoro ikiwemo eneo la Msomera.

Kwamba nyumba hizo 5000 zinatarajiwa kuchukuwa watu wa Kaya zilizopo Ngorongoro, huku Matinyi akiweka wazi kuwa Serikali hamzuii mtu aliyepo Ngorongoro kuhamia kwa hiari yake kwenye maeneo mengine ya Nchi na kusema kuwa eneo la Ngorongoro limekaliwa jamii ya Wamasai na kwamba pamoja na Wamasai kutawanyika katika mikoa takribani 14 ya Tanzania, lakini serikali ilichukua pori Tengefu la Handeni (Msomera) na kulitenga kwa ajili yao.

"Msomera kuna Tume Maalumu iliundwa na Wizara mbalimbali katika kufanikisha operesheni hii, Wizara hizo ni Wizara  Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI), Maliasili na Utalii, Nishati, Hbari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kilimo, Maji, Mifugo na Uvuvi, Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jinsia, Wanawake, Wazee na Makundi Maalum na Katiba na Sheria," amebainisha Matinyi na kusema,

"Kwahiyo nini kinafanyika pale Msomera, kufanya kazi ya kupima viwanja na kujenga nyumba, barabara, mifumo ya umeme, ambapo kila mwananchi ataunganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi 27,000 na TANESCO, Wizara ya Maji itajenga visima na kutakua na usambazaji ili yawafikie wananchi,".

Amesema kwamba kwa upande wa Wizara ya Mifugo imekwenda kujenga mnada wa kisasa ili wananchi wapate shughuli ya kiuchumi, likini pia imeongeza vituo vya kukusanyia maziwa. 

Msemaji huyo amesema shughuli za kiuchumi zinakwenda kuongezwa ili wananchi waweze kupata maendeleo na kwamba familia ambazo zimekwishahamia, kwa fedha walizolipwa na maendeleo wanayopata, wengi sassa wanamiliki vyombo vya usafiri mbali ya kwamba baadhi yao wameanza kujishugulisha na kilimo.

Hivyo ameeleza kuwa kwasababu Jamii ya Wafugaji sio wazuri kwenye kilimo, Wizara ya Kilimo imejipanga kuanzisha mashamba darasa ili kuwapa fursa ya kujifunza na hatimaye kulima kilimo cha kisasa chenye tija kiuchumi.

Awali akieleza sababu za kuwahamisha wananchi wa Ngorongoro, Matinyi amebainisha kuwa Tarafa ya Ngorongoro ina kata 11, na vijiji 25 ambavyo vilikuwa na  jumla ya wananchi 115,000, hali iliyosababisha Hifadhi ya Ngorongoro kumezwa kutokana na ongezeko la watu na mtawanyiko wa shughuli zao ndani ya eneo hilo.

Hivyo Serikali ikaona ni vyema kuliangalia suala hilo, pamoja na kwamba wananchi hao wanaishi wanaishi kwa kufuata masharti, likini ndani ya hifadhi wameshindwa kupata maendeleo ambayo Watanzania wengine wanayapata.

"Wakati Watanzania wengine wanapewa fursa za shughuli za kiuchumi, wanapewa mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi, lakini watu wa ndani ya hifadhi haiwezekani, wakati wanajengewa huduma za kijamii na miundombinu wale wa pale haiwezekani," amesisitiza Matinyi.

Kutokana na hali hiyo, Matinyi amesema maisha yao yameendelea kuwa duni wakiishi kwa kupatiwa msaada wa vyakula na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, lakini pia, uwepo huo wa watu umeathiri utalii kwamba Mtalii anapotoka huko kwao na kuja Tanzania, matarajio yake ni kuja kuona wanyamapori, lakini anapoingia katika Hifadhi ya Ngorongoro asilimia 44 ya eneo, anakumbana na maisha ya binadamu  na mifugo.

Kwamba takwimu zinaeleza kuwa kati ya mwaka 2015 hadi 2021, wanainchi waliopoteza maisha kwa kushambuliwa na kuliwa na wanyama ni 49 achilia mbali mifugo iliyouliwa na wananchi waliojeruhuwa na kusababishia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kutumia gharama kubwa kwa ajili ya matibabu ya watu hao. 

"Kwahiyo mgogoro huu wa maisha ya binadamu kuingiliana na wanyama, kushindwa kuwapa wananchi maendeleo, Hifadhi kuathirika, na utalii kuathuirika, ni Sababu za Msingi za Rais kuigiza Wizara ya Maliasili na Utalii na Mamlaka ya Hifadhi ya Enao la Ngorongoro kutafuta utatuzi wa suala hilo. Hivyo kukaanza kutafutwa eneo Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakaenda kuangalia Pori Tengefu la Handeni, na maeneo mengine yaliyotegwa likiwemo lililopo lililopo Simanjiro, yalipowekwa pamoja kukapatikana eneo kubwa tofauti na lile wanaloishi Ngorongoro," amesema Matinyi.

Hivyo maeneo hayo yakawekwa katika wa kuyaendeleza ili wananchi wakazi wa Ngorongoro kwa hiari yao wahamie na kufanya maendeleo ya kiuchumi na kujikwamua katika lindi la

Post a Comment

0 Comments