Na Sheila Ahmadi
Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli na Gesi Asilia (PURA) pamoja na Mamlaka ya udhibiti wa utafutaji na uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia Zanzibar (ZPRA) zimekutana na kuweka mipango mikakati mbalimbali Jijini Dar es saalam na kuweza kuendeleza sekta ya Mafuta na Gesi asilia Nchini na kuendeleza uchumi wa nchi
Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam katika mkutano huo alipokua akizungumza na wanahabari Mkurugenzi mkuu wa pura mhandisi Charles Sangweni ambapo amesema kuwa mkutano huo una Dhamira ya kuwa na mipango mahususi ya kukuza na kuendeleza sekta ya Mafuta na Gesi asilia kwa pande zote mbili za Muungano, na kuwekeana mikakati thabiti ya kutangaza na kutafta wawekezaji wa vitalu vya mafuta na gesi.
"Katika mkutano huu tumekutana ili tuweze kupanga mikakati katika kujengeana uwezo na kubadilishana uzoefu ili tuweze kudhibiti na kuendeleza sekta hii muhimu kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa letu,tunatumaini baada ya kikao hiki tutaainisha mikakati yetu na kuifanyia kazi ipasavyo" Amesema Mhandisi Sangweni.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya PURA Khalfan Khalfan ameongeza kuwa ushirikiano wa PURA na ZPRA utaenda kusaidia katika kujenga mahusiano ya muda mrefu na kwenda kuhakikisha kuwa wawekezaji wanapatikana Tanzania huku wakiendelea na ushirikiano katika kutoa huduma kwa wananchi wote.
Mwenyekiti Khalfan Amesema kuwa ushirikiano huo unaenda kuleta manufaa endelevu kwenye bodi zote mbili( PURA na ZPRA ) na kuwezesha kutaweza kutangaza vitalu vinginevyo na kuweza kupata wawekezaji wengi hivyo sekta ya Mafuta na Gesi asili itazidi kukua nakuleta maendeleo kwa Taifa." Amesema mwenyekiti Khalfan
kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi kutoka taasisi ya Utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar Ali Mirza amesema kwamba kikao hicho kimefanyika kwa mara ya kwanza ili kuweza kujadiliana kwa pamoja nakuweka mikakati ya pamoja ya kunufaika na rasilimali ya Mafuta na Gesi asilia.
Ameongeza kuwa ushirikiano huo unaenda kuleta tija kwenye bodi zote mbili PURA na ZPRA na kuweza kutangaza vitalu vyote katika kuvutia wawekezaji wengi nchini hivyo sekta hiyo ya mafuta na gesi asili inaenda kuleta manufaa kwa Taifa.
0 Comments