Na Mwandishi wetu
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Judith Kapinga amewaalika Wanawake kutoka maeneo mbalimbali nchini kushiriki katika kongamano kubwa la Wanawake la Nishati Safi ya kupikia litakalofanyika jijini Dodoma ambalo limeandaliwa na Wizara ya Nishati.
Kongamano hilo litafanyika tarehe 9 Machi, 2024 ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani pamoja na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.
0 Comments