Na Sheila Ahmadi
Waziri wa Ardhi nyumba ,maendeleo na makazi Mhe Jerry silaa amesema kuwa bado wanaendelea na zoezi la urasimishwaji wa ardhi maeneo mbalimbali nchini huku matapeli papa kutoka mkoa wa dar es salaam wakaamatwa huku matapeli wawili wa ardhi tumeanza kuwafanyia kazi maalumu.
Akizungumza jijini Dar es salaam Waziri wa Ardhi Mhe.Jerry silaa amesema kuwa wizara yetu imepokea maelekezo kutoka kwa Mh Rais Dkt samia suluhu hasani ni kwenda kuhakikisha kuwa migogoro ya ardhi ambayo inatokea iweze kuisha kwa haraka hivyo hatuwezi kuwaachia wananchi waendelee kumaliza kesi hizi kiholela wakati serikali Ipo wakati wowote.
Kwakuwa matapeli hao wa ardhi wana mbinu nyingi wanatumia katika kutapeli ardhi za watu mbalimbali huku wakitumia nguvu,ubabe,na pesa zap hivyo inapeleka wananchi kukosa haki zao za msingi mkoani Dar es salam maeneo ya mbezi beach kulitokea na kesi ploti namba 911 na wananchi wengi wamekuwa wakituma ujumbe mara kwa mara ili waweze kusaidiwa suala hilo la matapeli wa ardhi " Amesema waziri Silaa"
"Kwa sasa tumeamua kufanya oparesheni maalumu mkoani dare salaam kwani oparesheni hii tutaenda kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kwenda kuweza kuhakikisha tatizo hilo linafikia kikomo pia naomba kuwahakikishia watanzania kuwa ni nchi yenye usawa hivyo hakuna mtu yoyote ambaye atachukua haki ya mtu mwingine hivyo tumeamua kufanya hivyo na kuwasaidia wananchi katika suala la Ardhi.
Kwa upande wake Afisa Ardhi kutoka daraja la kwanza ndugu Jacob ngowi amesema kuwa wanachi wote wanatakiwa kutoa maoni yao na kuwa huru pindi migogoro ya ardhi inapotokea waweze kuleta nyaraka husika kwenye ofisi zetu jijini Dar es salaam na nipo muda wote kuweza kuhudumia wananchi wetu ipasavyo kwani serikali yetu imeweza kutuamini kwa utendaji wetu wa kazi kupitia sekta ya ardhi.
Naye Mmoja wa wadhulumiwa kiwanja kutoka Mkoa wa Dar es salam ameitaka wizara hiyo iweze kumrejeshea kiwanja chake kwani ni muda mrefu umepita tangu kwani kwa sasa nahitaji kupatiwa kiwanja changu ili niweze kufuta kesi hii maaana kuna watu wawili walinidhulumu kiwanja changu kwa muda mrefu ambao ni Tarimo na mushi.
Aidha kuna risiti ambazo na barua zote husika za wizara nimehifadhi kwani kuna visibitisho vyote muhimu ambavyo vinaweza kuleta ushahidi wa kuweza kupata kiwanja changu hivyo naomba serikali ya awamu ya sita iweze kutatua suala hili kwa wakati kwani ni jambo ambalo limekua changamoto kwa baadhi ya wananchi kutapeliwa na kulagai viwanja vyetu.
0 Comments