Na Sheilla Ahmadi
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana amesema Uhusiano na Ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na Urusi haujaanza leo, bali ulianza zamani kipindi cha uongozi wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Hivyo Dkt. Pindi Chana amesema hayo Jijini Dar es saalam alipokuwa akizungumza katika mafunzo yaliyofanyika katika Taasisi ya Uanasheria kwa Vitendo (LST)
" umuhimu wa mkutano huo, Balozi Dkt. Pindi Chana amesema wanafunzi wa sheria kwa vitendo walioshiriki katika mhadhara huo watapata faida kubwa kwa kulinganisha mambo mbalimbali ya kisheria wenzao Urusi wanayatatuaje katika harakati za kujiweka salama, kisheria na kiuchumi.
Aidha. Dkt chana amesema kuwa mkutano huu unafanyika kwa ajili ya kuweza kudumisha na kutekeleza falsafa ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika 4R kuna moja inayohusu jambo linalofanyika hapo leo, na kusema nchi lazima ishirikiane na nyingine ili kupata ushirika na uzoefu kutoka kwa wageni.
Dkt. Chana amesema mikutano kama hii hufundisha wanafunzi wa fani mbalimbali na kuleta ufahamu na weledi katika masomo yao wanayofanya kwa vitendo kwa manufaa ya taifa kwa ujumla." Amesema dkt chana.
“Urusi ni wazuri wa mambo ya Teknolojia katika ulinzi na usalama kisheria hivyo vijana hao wakipata kujifunza kutoka kwa Wataalam wataongeza ujuzi na kuutumia siku zijazo kwa manufaa yao na nchi yao” ameeleza Dkt. Pindi Chana.
Vilevile , Dkt. Chana amesema wageni hao wametoka Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Urusi kutembelea Tanzania kwa shughuli za kujifunza na kudumisha uhusiano na ushirikiano ulikuwepo hata kabla ya Uhuru nchini.
Mkutano huo uliofunguliwa na Mhe. Pindi Chana umehudhuriwa na wanafunzi wa taasisi hiyo, wataalam kutoka Urusi na wageni mbalimbali waalikwa bila kusahau wahadhiri mahiri katika taasisi hiyo.



0 Comments