Na Sheila Ahmadi
Serikali inaendelea kutokomeza ugonjwa wa Malaria nchini kutoka Mwaka 2020 mpaka ifikapo 2030 kupitia Taasisi ya Afya kutoka ifakara ambayo imefanya kongamano la Malaria foramu jijini dar es salaam huku ikihusisha viongozi mbalimbali nchini kutoka wizara ya Afya wakiwemo wabunge ikiwa na lengo la kutokomeza ugonjwa huo wa malaria kidunia.
Akizungumza jijini Dar es salaam Mganga Mkuu wa serikali professa Tumaini Nagu Amesema kuwa shirika la ifakara la Afya zimeweza kukusanya utafiti mablimbali ambao wanaungana katika kutafakari juu ya kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini hivyo leo wameweza kukutana na watafiti wa Malaria kwani tumeona kwa ambao umepita na sass hivi ni tofauti kutokana na ongezeko la Mvua nyingi zinazonyesha nchini.
"Tumeona mabadiliko ya nchi yanapelekea kuongezeka kwa ugonjwa huo wa Malaria hivyo tumeona ongezeko kiasi kwani kuna changamoto ambazo zimejitokeza kwa kipindi cha maiaka hii miwili kwani matumizi ya Teknolojia itatengeneza njia za kudhibiti ugonjwa huo. Ikiwemo mabadiliko ya Tabia ya nchi na kwenda kuhakikisha kuwa tunatahadharisha kwa wananchi kwa kuzuia malaria .
Aidha Professa Nagu amesema tuko kwenye kutafuta mbinu mbadala ya kujikinga na malaria na tuna uhaba wa dawa za malaria na tunakabiliana nalo kabula ya halijakuwa kwa sana nchini kwetu Natoa wito kwa wataalamu wa malaria katika kuweza kutumika Teknolojia katika kupambana na malaria lakini wanasayansi na watafiti wahakikishe kuwa wanatafuta mbinu mandala katuka kuweza kutokomeza malaria. Amesema Profesa Nagu.
Tunajua tuna changamoto ya Fedha lakini vyanzo ambavyo tunazo tunatakiwa kutumia vizuri ili tuweze kuwa na kipaumbele kwa mambo ambayo yana tija
Ikiwemo utunzaji mzuri wa dawa hivyo Mwaka tumepiga hatua kubwa Katika kupunguza malaria kufikia aslimia 65 huku Mwaka 2023 vifo vya malaria vikiongeza .
Naye mkurugenzi wa Taasisi ya Afya ifakara Honorati Masanja amesema kuuwa tumepokea Maelekezo kutoka kwa mganga mkuu wa serikali kuwa tutumie Teknolojia ya Akili bandia Katika kuweza kupambna dhidi ya malaria kwani ulimwengu wa sasa hivi unaenda kwa matumizi mengi ya Teknolojia .
Kwa sasa tumeanza kutumia Teknolojia ya AI zinatumika kwenye matumizi ya vyandarua huku vikiwa na mwisho wa matumizi Kwa wakati gani inafaa kwa matumizi ya binadamu na tunafanya ukaguzi wa matundu hayo Katika kuweka usalama wa matumizi ya vyandarua .
Kwa upande wake Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndungulile amesema kuwa malaria inatibika na tunataka mpaka kufikia Mwaka 2030 tuwe tumetokomeza kwani mmbu kwa sasa wamebadilisha tabia zao kipindi cha nyuma walikua wanapiga kelele ila kwa sasa hawapigi na tunatakiwa kutumia vyandarua vyenye dawa ili kutokomeza vifo, vitokanavyo na mmbu nchini.Amesema mbunge Ndungulile.


0 Comments