JUMIKITA , TRA YATOA ELIMU KWA WANAHABARI WA MITANDAO YA KIJAMII. KWENYE SUALA LA ULIPAJI WA KODI.

 

Na  Mwandishi wetu

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA kwa kushirikiana na Jumuiya  ya mitandao ya kijamii nchini Tanzania  JUMIKITA imetoa elimu   kwa wanahabari wa mitandao ya kijamii  Tanzania  kuhusu  ulipaji wa kodi nchini  ili kuweza  kupata huduma na kuweza kuhakikisha wananchi wanapata risiti baada ya kufanya manunuzi pindi wapatapo huduma.


Akizungumza jijini Dar es salaam  kaimu mkurugenzi. Mtendaji wa elimu ya mlipa kodi  na Mawasiliano TRA  Hudson kamoga mara baada ya kufungua semina hiyo amesema kuwa  makusanyo ambayo yanapatikana katika ulipaji wa kodi ni maelekezo kutoka kwenye serikali yetu tunafanya hivyo katika kuweka maendeleo ya nchi kupitia kwenye kodi ambazo zinalipwa na wananchi.


Kulipa kodi ni muhimu kwa kila mtu kwani inaenda kuleta mapato ya  nchi ambayo yanaenda kuleta maendeleo nchini hivyo tusipolipa kodi kwa.wakati tutakuwa tunadumaza maendeleo ya nchi katika.mapato hayo yatokanayo na ulipaji wa kodi hizo ambazo zinalipwa kwenye sekta mbalimbali." Amesema mkurugenzi  kamoga".


Kama TRA tunaahidi tutakuwa bega kwa bega na ninyi, na tunafanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha tunamsaidia Rais kufanikisha mipango ya Maendeleo kupitia ukusanyaji Kodi,” amesema Kamoga na kuongoza,


“‘Forum’ hii sio ya mwisho tutaendelea kukutana, hivyo tupo tayari kwa ushirikiano na ni imaini yangu hata kwa waandishi wa Habari wa Mitandao ya Kijamii wa mikoani tutakutana nao ili nao waweze kupata uwezeshaji huu,”.


Akieleza sababu ya TRA kukutana na Waandishi wa Habari wa Mitandao ya Kijamii, Kamoga amesema ni kutokana na  maelekezo ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Alphayo Kidata ya kutaka elimu ya Mlipakodi inawafikia Watanzania wote.


Kwamba pamoja na sababu hiyo ni kuimarisha ushirikiano na Jamii kupitia waandishi hao ikizingatiwa kuwa kupitia mitandao ya kijamii Dunia imekuwa kama Kijiji, hivyo TRA wakiitumia itakuwa rahisi elimu ya Mlipakodi kuwafikia watu wengi kwa haraka.


Kamoga ameongeza kuwa kutokana na Maendeleo ya Kidigitali, huwezi kufanikiwa bila kushirikisha waandishi wa Habari wa Mitandao ya Kijamii.


Hata hivyo wametumia fursa hiyo kuwapa elimu ya masuala mbalimbali ya nayohusu TRA ikiwemo makusanyo ya Kodi ya Kidigitali, umuhimu ya kudai risti unapofanya manunuzi, mambo ya forodha, EFD, ETS na huduma kwa mteja.k


“Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii wakijua haya ni rahisi wananchi kupata taarifa sahihi za TRA, hivyo tukaona ni muhimu tukutane nanyi,” amesisitiza Kamoga.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa JUMIKITA Shabani Matwebe ameipongeza TRA kwa kuwa Taasisi ya kwanza ya Serikali kutambua na kuthamini nguvu ya mitandao ya kijamii.


“TRA ni Taasisi ya kwanza kugundua nguvu ya Digital Platform, Nyie mnajua ni jinsi gani mnapata tabu kupata taarifa ikitokea mtu amewatambua ni lazima tumpongeze, Digitali Platform haikwepeki, Mkurugenzi nikupongeze,” amesema Matwebe.


Post a Comment

0 Comments