Na Sheila Ahmadi
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt samia suluhu hassani anaenda kufanya Ziara ya kikazi. Nchini korea huku ziara hiyo ikiwa na dhamira ya kuendeleza ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Korea ikiwemo Elimu, Afya, na miundombinu hivyo ziara hiyo inaenda kuleta Mafanikio mbalimbali nchini kwetu. Tanzania
Hayo Yamesemwa Jijini Dar es salaam na Waziri. Wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki January Makamba mara baada ya kuzungumza na wanahabari ambapo amesema kuwa tarehe 30 mwezi huu Rais Dkt samia atafanya ziara nchini korea hadi tarehe sita kwa mwaliko rasmi kutoka kwa rais wa nchi hiyo kwani sisi na watu wa korea tuna ushirikiano mkubwa kwa miaka 32.Kupitia Elimu, Afya, na Miundombinu.
Kwenye ziara hiyo Dkt samia atafanya mazungumzo na kusaini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Korea mikataba hiyo ikiwemo Hati ya makubaliano kati ya Taasisi ya Madini Tanzania. GST na Taasisi ya miamba nchini korea. Hivyo ushirikiano huo unahusu utafiti, uchoraji ramani, rasilimali na uchoraji wa maabara .
"Mkataba wa pili ambao unaenda kusainiwa kati ya Rais Samia na rais wa korea ni ushirikiano wa uchumi. Wa bluu, huku mkataba wa tatu ukihusu kwenda kutambua vyeti vya Mabaharia na tutaweza kusaini Tamko la pamoja kuhusu siasa na makubaliano ya hati ya Madini, Viwanda na biashara " Amesema Waziri makamba
Aidha Waziri Makamba ameongeza kuwa kuhusu madini kwenye mkakati tutasaini mkataba katika kuwezesha kuchambua, na Kufanya Mkakati na shirika la madini Tanzania STAMICO , na shirika la ukarabati wa madini nchini korea
Hata hivyo Mkataba mwingine ni Msaada wa fedha kutoka benki ya Exim nchini korea na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao unaenda kupelekea nchi yetu kupata msaada na mikopo nafuu Takribani dola mbili nanusu vilevile tunaenda kushirikiana na chuo kikuu kutoka nchini korea katika kuendeleza. Huduma za usafiri wa anga nchini

0 Comments