Na Mwandishi wetu.
Kampuni ya Heineken Imetanagza rasmi kununua. Kampuni ya Dustell na namibia breweries ambapo inaenda kuzindua jarida jipya la vinywaji vya heineken kwani dhamira ya kampuni hiyo ni kuweza kuwasilisha vinywaji vya ubora wa hali ya juu kwa watumiaji mbalimbali barani kote.
Akizungumza jijini Dar es saalam Meneja mkazi nchini kutoka kampuni ya Heineken Obabiyi fagade amesema kuwa katika mapato halisi na euro milion 150 katika faida ya uendeshaji wa nyayo zetu za afrika unachangia kwa kiasi kikubwa hivyo ukuaji wa uchumi nchini Tanzania unaongezeka.
"Sisi tumepewa nafasi ya kipekee katika kuwafikia hadhira zaidi kutokana na upanuzi lakini tunaendelea kutengeneza nafasi nyingi za kazi na kuwawezesha watanzania wengi zaidi.
Aidha meneja fagade amesema kuwa Heineken kwa sasa inapatikana katika masoko 114 nchini na kuuzwa katika masoko zaidi ya 180 na ikiwa tayari katika tasnia ya vinywaji nchini Tanzania huku maadili na misingi katika kutoa furaha kwa wateja wake na watumiaji ili kwenda kuhamasisha ubunifu na ufanisi." amesema meneja Fagade"
Kwa upande wake Meneja wa Masoko na biashara kutoka kwenye kampuni ya Heineken. Lilian Pascal amesema kuwa katika hafla hiyo tutakuwa na Waziri wa mipango na uwekezaji Prof Kitila mkumbo ikiwa na lengo la kuadhimisha kinywaji hicho cha Heineken.
Vilevile Ameongeza kusema kuwa Heineken ni moja ya Kampuni kuu ya vinywaji ulimwenguni katika kusambaza bidhaa hizo kwa watumiaji hivyo kutokana na uwepo wake wa kinywaji hicho katika masoko 114 pamoja na mauzo katika masoko 180 na kuendelea kuvumbua jalada lake ni kuweza kukidhi mahitaji mbalimbali kwa wateja wake.

0 Comments