WIKI YA UBUNIFU KUFANYIKA DAR ES SALAAM NA KILELE CHAKE KUISHIA MKOANI TANGA.



Na mwandishi wetu

Kuelekea wiki ya ubunifu serikali kuendelea kuboresha mazingira ya sekta ya hiyo kwa kuhakikisha kuwa teknolojia na bidhaa zinazobuniwa na Watanzania zinaweza kushindana na bidhaa kutoka mataifa mbalimbali Duniani.


Hayo yameelezwa   Jijini Dar es Salaam katika Mdahalo na Waandishi wa habari kuelekea Wiki ya ubunifu Tanzania itakayoanza rasmi Mei 21/2024 ambapo Mkurugenzi Huduma za Sayansi na Teknolojia Kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Ladislaus Nyoni, amesema bunifu mbalimbali zitasaidia kuongeza ajira na kutatua changamoto za watanzania.


Aidha ameongeza kuwa serikali inahakikisha kuwa inawasaidia vijana wabunifu kutengeneza wigo mpana wa kutumia bunifu hizo kutatua changamoto zilizopo nchini na kukuza uchumi.

Kwa  upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu ametoa wito kwa watanzania na wadau mbalimbali kushiriki wiki ya ubunifu katika ukumbi wa Mikutano Kimataifa wa Julius Nyerere  Jijini Dar es salaam,(JNICC) ambapo kutakuwa na maonyesho mbalimbali ya bunifu za kisayansi na teknolojia.


Ameongeza kuwa wiki ya ubunifu ilianzishwa na COSTECH na baadae ikaitwa HDIF na kwasasa ni program ya Ubunifu wa FUNGUO ambapo moja wapo ya mafanikio ya mradi huo ni kuanzishwa kwa Mashindano ya MAKISATU.


Hata hivyo kupitia Jukwaa hilo la Wiki ya ubunifu limekuwa na mijadala mbalimbali inayochagiza maendeleo katika sekta ya ubunifu hususani kwa vijana na kusavutia wengi zaidi, pia amesema wiki ya ubunifu imekuwa ikiibua vipaji mbalimbali vya ubunifu.


Naye  Meneja wa program ya Funguo Joseph Manirakiza amesema kuwa katika wiki ya ubunifu tujionea nguvu ya mabadiliko kupitia teknolojia na ubunifu na tukio hili ni hatua ya kuelekea wiki ya kitaifa ya elimu,ujuzi na ubunifu kwa kuangazia vitu muhimu katika sekta.


Pia amesema Mwisho wa maadhimisho ya wiki ya ubunifu kutakuwa na tuzo za kuwatambua wabunifu mbalimbali waliofanya vizuri ambapo wiki ya ubunifu itatamatika mei 24/2024.


Mwakilishi wa Ubalozi wa umoja Ulaya Janet Mortoo Amesema Vyombo vya habari ni daraja katika jamii la wananchi kupata taarifa muhimu kutoka sehemu mbalimbali,vyombo vya habari ni chanzo kikuu cha taarifa na maarifa hivyo 


Kupitia ubunifu vyombo vya habari vinaweza kusaidia zaidii katika kufikia malengo yanayotakiwa na vijana wengi wakafaidika zaidi na bunifu zao kwa kupata taarifa sahihi kuhusu ubunifu kupitia Vyombo vya habari.

Post a Comment

0 Comments