KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania na kampuni ya kutengeneza simu ya itel leo kwa pamoja wameshirikiana wamezindua simu mpya ya itel A80 iliyoambatanishwa na ofa ya bando ya intaneti yenye kifurushi cha BURE cha GB 75 ambacho kinadumu kwa muda wa miezi kumi na mbili.
Ushirikiano wa Airtel na itel unawahakikishia Watanzania uwezo wa kupata simu za kisasa za smartphone zenye ubora wa juu kwa gharama nafuu zaidi.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja Mahusianokutoka Airtel Tauzania Jennifer Mbuya, uzinduzi wa simu hiyo unaonyesha ari ya Airtel Tanzania katıla kupunguza mgagawanyiko wa kidigitali nchini kupitia teknolojia suluhishi kwa bei nafuu.
"Ushirikiano wetu na itel utaongeza matumizi ya simu kwa watumiaji wa Airtel kote nchini
kwa kuchanganya vipengele vya kisasa vya ltel na mtandao bora wa Airtel wenye kasi zaidi. Ushirikiano huu unaonyesha jinsi tunavyojitolea katika kurahisisha maisha ya
wateja wetu kupitia bidhaa za kibunitu," alisema.

0 Comments