#KAZIINAONGEA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan amewatakia kheri wanafunzi wote wa Kidato cha Nne ambao leo wameanza rasmi Mtihani wa Kuhitimu (CSEE).
"Nawaombea utulivu na mafaniko katika hatua hii muhimu ya kujiandaa kushiriki vyema kwenye nguvu kazi ya familia, jamii na Taifa kwa ujumla.
Mafanikio yenu katika hatua hii yatakuwa pia faraja kwa waalimu, wazazi na Watanzania wote ambao kupitia ulipaji kodi na utunzaji wa amani na utulivu wa nchi yetu wanaiwezesha Serikali kuendelea kutekeleza mipango tunayojiwekea, ikiwemo kutoa elimu bure kuanzia Darasa la Kwanza hadi Kidato cha Sita, na kazi mpya tuliyoanza ya kuboresha mfumo wetu wa elimu ili uendane na mazingira na mahitaji ya sasa.
Mwenyezi Mungu awaongoze na kuwasimamia". Ameandika Rais Samia.

0 Comments