BITEKO AFUNGUA MAONESHO YA SITA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA DSM.

Naibu Waziri Mkuu Mhe.Dotto Biteko alimwakilisha Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan,katika Kongamano na Maonesho ya tisa ya kitaifa ya sayansi na teknolojia na ubunifu yaliyofanyika hapo jana(November2)alisema kwamba

“Serikali inathmini sana mchango wa tafiti zenu na imeendelea kuimarisha masuala mbalimbali ya utafiti”
Pia aliongezea kwa kusema “Serikali inatekeleza mradi wa heat wa tirion 1.53 ambapo moja wapo ya matumizi ya fedha hizo ni kukukarabati majengo 370,na maabara 563”
Vilevile “Vituo zaidi ya 50 vya ubunifu na utafiti vimeimerishwa na vimechangia zaidi ya ajira 100 na Bado tunahitaji kuweka nguvu kubwa katika sayansi na kuwapa fursa watafiti ili kupata majibu ya changamoto zetu kwa sababu matatizo tuliyonayo yatatuliwa kupitia sayansi na tafiti ambazo tumezifanya”
“Serikali yetu imefanya mambo mengi,kama kuna ajenda kubwa ambayo wizaara imeipa msukumo mkubwa ni tafiti na ubunifu”alisema Biteko
Naye Mkurugenzi mkuu wa COSTECH Dkt Amos Nungu alisema kwamba 
“Tume yetu ilizinduliwa rasmi mwaka 1988 na ni taasisi ya muungano ambayo inashughulikia masuala makubwa ya serikali ikiwemo tafiti na ubunifu”
“Tumefanikiwa kuimarisha mifumo nya utafiti na kuendeleza utafiti hapa nchini na tunamuongozo wa kitaifa wa ubunifu ambao tumetoa vibali vya ubunifu zaidi ya 100 na   tunashirikiana nan a mashirika kama UNDP,WFP na UNICEF ambao tumefanya nao kazi kwenye utafiti na ubunifu”alisema Nungu
Na alimalizia kwa kusema “pia tunaishukuru serikali katika kugharamia tafiti sera za nchi yetu ya kufungua nchi,hiyo imetuwezesha kufanya diplomasia ya sayansi, na ubunifu,tumepokea fedha  Norway na tutapokea fedha sweeden kwa ajili ya tafiti na ubunifu”


Post a Comment

0 Comments