Naibu Waziri Mkuu na Waziri Wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko (MB.), amesema Serikali inatambua kazi inayofanywa na TCCIA katika kuchochea maendeleo ya biashara nchini, Dkt. Biteko ameayasema hayo leo jijini Dar es salaam akifungua “Mkutano wa Mwaka wa Majadiliano ya Biashara na Uwekezaji kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kwa mwaka 2024, ulioandaliwa na TCCIA kwa kushirikiana na TradeMarkAfrika Kampuni ya Kamaka pamoja na wadau mbalimbali, Majadiliano ya Mkutano huu yamebeba kauli mbiu isemayo “Kuongeza Ufanisi wa Majadiliano na ushindani wa Mauzo ya Nje kwa Ustawi wa Sekta Binafsi”. Akizungungumza katika hotuba yake, Dkt. Biteko Alisema.
“Ninataka kutumia fursa hii kuipongeza TCCIA kwa kuandaa Mkutano Mkuu wa 49 wa mwaka 2024 na kuendelea kuwa mstari wa mbele kuendeleza sekta binafsi hasa iliyojikita katika sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi, viwanda na biashara. Sisi ambao tumekuwa tukifanya kazi kwa karibu na sekta binafsi, tunaamini kuwa sekta binafsi ni injini kuu ya kukuza uchumi wa Taifa lolote. Ndiyo maana mliponialika kuwa Mgeni Rasmi kwenye mkutano huu, sikusita kuja kushiriki pamoja nanyi.”
Aliongeza, “Ninawashukuru sana kwa mwaliko huu na, kama ambavyo mnajua, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania iko tayari kuendelea kushirikiana na sekta binafsi ili kuhakikisha nchi yetu inaendelea kupiga hatua za maendeleo.”
0 Comments