MKURUGENZI MTENDAJI WA TCCIA NDUGU OSCAR KISANGA ATOA TAARIFA YA UTEKELEZAJI YA MWAKA 2024.



Ndugu  Oscar kisanga ,Mkurugenzi mtendaji  wa Chemba ya Biashara, Viwanda na kilimo Tanzania (TCCIA)akizungumza katika mkutano wa 49 wa Mwaka 2024 leo jijini Dar es salaam alisema kwamba  "Ushiriki wenu ni msingi wa Dola mpya TCCIA,mkutano wa mwaka wa sekta ya uwekezaji unalenga katika kujadili maendeleo ya kilimo,viwanda na biashara"
Na umewakutanisha wanachama na wadau kutoka miko 26 Tz bara,Katika kipindi cha miaka 36 cha kusimamia na kukupa sekta binafsi TCCIA imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali,pia imejikita kuleta mbadaliko ya kiuchumi"alisemaKisanga.
Na aliongezea kwa kusema "Katika kuunga mkono Dira hiyo TCCIA imekuwa ikitoa vyeti vya asili vya bidhaa,na kujenga maendeleo endelevu yenye uchumi imara,pia nimpongeze Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuunda tume ya mabadiliko ya kodi"
"Eneo la kwanza ni uwezeshwaji wa biashara,kampuni 70 zilifanya mafunzo ya kushiriki katika soko la afrika,na utoaji wa vyeti vya uasili,takwimu za January hadi December 51.8%vilitolewa kieletroniki.
"Ukaguzi wa bidhaa za viwandani,TCCIA imefanya ukaguzi wa viwanda 36 ambapo bidhaa 47 zilithibitishwa,Na TCCIA ilishiriki misheni NNE za biashara katika nchi za Indonesia,ubelgiji na uingereza" vilevile Kikao cha majadiliano na mabalozi katika eneo la biashara na uchumi,kikao hicho kilileta chini ya washiriki 250. 

Post a Comment

0 Comments