KIBAHA MJI YAFANYA KWELI KUZINDUA RASMI SOKO KUBWA LA KISASA DISEMBA 7


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 


Halmashauri ya Kibaha mji iliyopo Mkoa wa Pwani kesho  inatarajia kuzindua rasmi soka jipya la kisasa linalojulikana kama (Kibaha Shoping Moll) Novemba 7 mwaka huu lililogharimu kiasi cha shilingi bilioni 7.


Akizungumza na waandishi wa habari Afisa mapato wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Luna Kakuru  amebainisha kwamba  mradi huo ni kati ya miradi ya kimkakati na kwamba fedha hizo zimetolewa na Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan


Luna amesema kwamba katika mradi huuo  wanategemea baadae mapato kuongezeka zaidi kutokana na huduma zitakazoendelea kutolewa ikiwepo maeneo ya maegesho ya magari.


 Naye Afisa Masoko wa soko hilo Sabrina Kikoti amesema katika ufunguzi huo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John na kwamba soko hilo litakwenda  kufungua fursa za  uchumi kwa wananchi wa Kibaha pamoja na maeneo mengine.


Sabrina ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha hizo ambazo zimetekeleza mradi huo unaokwenda kutoa huduma nyingi  huduma nyingi ambazo wananchi walikuwa hawazipati kwa wakati.


Amesema katika ufunguzi huo wafanyabiashara mbalimbali wakubwa watashiriki wakiwemo wasanij kutoka ndani na nje ya Mji wa Kibaha.


Nao baadhi ya wafanyabiashara akiwemo Charles Chandika  amesema kwamba uwepo wa soko hilo ni fursa kwa wafanyabiashara kutoa huduma mbalimbali kwa wakazi wa mji huo kwa gharama nafuu.


Naye Lidya Vicent mfanyabiasha wa nguo katika soko hilo amesema uwepo wa soko hilo umewawezesha kupata fursa ya mahali sahihi pa kuuzia bidhaa zao.








         

Post a Comment

0 Comments