DC KHERI JAMES ASISITIZA UMUHIMU WA UWAJIBIKAJI KATIKA KUONGOZA VIJIJI NA MITAA.

 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Komred Kheri James, amewahimiza Wenyeviti wa vijiji na Mitaa katika wilaya ya Iringa kuwajibika kikamilifu ili kuchochea maendeleo na kujenga ustawi wa Mitaa na Vijiji vyao.              







Komred Kheri James ameyasema hayo mapema leo katika kikao kazi maalumu cha kuwajengea uwezo Wenyeviti na kutoa maelekezo ya Serikali, kilichofanyika mapema leo katika Ukumbi wa Mkuu wa wilaya ya Iringa.                                                         


Akizungumza katika kikao kazi hicho, Komred Kheri James amewahimiza Wenyeviti hao kufanya kazi kwa Uaminifu, uadilifu, ubunifu na uwajibikaji ili kuleta mageuzi ya kweli katika maeneo wanayo yaongoza.                                                 


Aidha Komred Kheri James amewasihi Wenyeviti wote kuhakikisha kuwa wanasimamia kikamilifu suala la Usalama, Miradi ya maendeleo, kusikiliza kero za wananchi, Kusimamia usafi na utunzaji wa Mazingira na kuusimamia kikamilifu suala la mapato katika maeneo yao.                   


Akihitimisha hotuba yake katika kikao kazi hicho Komred kheri James amewataka viongozi wote kuhakikisha mipango na maamuzi yao inaendelea kujenga misingi ya Haki, Usawa, Utawala wa sheria, maendeleo na Umoja na mshikamano.                                            


Kikao kazi hicho kimehudhuriwa na Wakurugenzi wa Halimashauri zote za Wilaya ya Iringa, Maafsa Tarafa, Kamati ya Usalama na Wenyeviti wa vijiji na Mitaa yote.

Post a Comment

0 Comments