MWAKA 2025 UTAKUWA NI MWAKA WA MAGEUZI NCHINI - ACT WAZALENDO

Waziri Mkuu Kivuli wa ACT WAZALENDO  alisisitiza hitaji la kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi, akibainisha kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 umeonesha sura halisi ya Rais Samia kuwa hataki mageuzi, kauli za R4 ni hadaa.

“Ili tuwe na uchaguzi wa haki na uwazi mwaka 2025, ni lazima tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi itakayohakikisha kila kura ya Mtanzania inaheshimiwa,” aliongeza.

Amehitimisha kwa kuahidi kuwa Baraza Kivuli litaendelea kuwa sauti ya wananchi, huku ikisisitiza mshikamano wa kitaifa kupambana na changamoto zilizopo. Huu ni mwaka wa kuchukua hatua thabiti. Tanzania inastahili zaidi ya haya tunayoshuhudia sasa. Ni wakati wa kuleta mageuzi ya kweli.

Post a Comment

0 Comments