Jafo awaomba Watanzania Kuwekeza UTT AMIS

 

Na Francisco Peter, Dar es Salaam 


Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Suleimani Jafo, amezitaka amewaomba Watanzania wawe wawekezaji wa UTT AMIS ambaye ni Mshirika Haki kakatika Uwekezaji  wakati lengo likiwa ni kuwezesha wananchi kujiweka akiba na kuwekeza katika masoko ya Fedha na mitaji.


Akizungumza mwisho wa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Haki za Watumiaji Duniani, Dkt. Jafo amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya mamlaka mbalimbali za udhibiti ili kuhakikisha bidhaa na huduma zinazopatikana zinakidhi viwango vya ubora na zinauzwa kwa bei nafuu.


Dkt. Jafo amezihimiza taasisi kama Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Vipimo (WMA), Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na taasisi nyingine muhimu kushirikiana kwa karibu ili kuimarisha ulinzi wa walaji.


“Haki za watumiaji ni nguzo muhimu kwa ustawi wa uchumi wetu. Serikali ina jukumu la kuhakikisha kuwa watumiaji wanalindwa dhidi ya unyonyaji, hasa katika mazingira ya mabadiliko ya soko la kimataifa,” alisema Dkt. Jafo.


Kwa upande wake Doris Mlenga ambaye ni Afisa Masoko wa UTT AMIS  amesema kunaunafuu muzuri katika kufikia malengo makubwa ya kibiashara kama fedha za wafanya biashara watawekeza  kuzitawanya katika sehemu mbali mbali wakijiwekea namna ya kuzitawanya kushiriki nasi  ambapo tayari watakuwa katika mazingira mengine yenye faida kwao .


Doris amesema kuwa kwa upande wa wafanya kazi ulalamika fedha za mishahara kuwa hazitoshi mara nyingi mishahara ujenga tabia ya kutuendesha sisi wafanya kazi ila endapo watawekeza katika mifuko yetu ni rahisi kuondokana na changamoto hiyo.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), William Erio, amesema kuwa FCC inaendelea kuchukua hatua madhubuti kulinda maslahi ya watumiaji na kuimarisha ushindani wa haki katika soko.


“Tunajivunia juhudi za kimataifa zinazolenga kulinda haki za walaji, na hapa Tanzania, tunahakikisha soko letu linakuwa la haki, uwazi na lenye ushindani wa kweli,” alisema Erio.


Aidha, alibainisha kuwa FCC imepata cheti cha Shirika la Uthibitisho la Kimataifa (ICO), hatua inayothibitisha jitihada za tume hiyo katika kupata utambuzi wa kimataifa na kujenga imani katika soko la Tanzania.


Post a Comment

0 Comments