HALMASHAURI KIBAHA MJI YAACHA GUMZO KUBWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KUPITIA MAPATO YA NDANI



VICTOR MASANGU, KIBAHA

 

Halmashauri ya Kibaha mjini kwa kushirikiana na baraza la madiwani kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025 imeweza kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo katika nyanja mbali mbali ambayo baadhi yake imetekelezwa kutokana na fedha zilizotolewa na Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan na nyingine zimetokana kupitia makusanyo ya mapato ya ndani.


Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha mjii Mhe. Mussa Ndomba wakati wa kikao cha mwisho kikanuni cha baraza la robo ya chenye lengo la kuweza kutoa taarifa ya utekelezaji wa mafanikio mbali mbali ambayo yametokea kwa kioindi cha mwaka wa kuanzia 2020 hadi kufikia mwaka 2025 ambapo wamebainisha mambo ambayo wameweza kuyafanya katika maeneo yao na jinsi walivyoweza kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo na kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha Mwenyekiti huyo akizungumzia mafanikio ambayo yamepatikana katika sekya ya afya amebainisha kwamba miradi miradi mbali mbali imefanyika ikiwemo ujenzi wa vituo viwili vya afya pamoja na zahanati tisa sambaamba na kupeleka vifaa tiba mbali mbali katika kituo cha afya mkoani na kuhakikisha inapeleka huduma ya maji safi na salama katika hospitali ya Lulanzi.


 Kwa upande wake aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ambaye pia ni Diwani wa kata ya Visiga Kambi Legeza amebainisha kwamba kwa kipindi cha miaka mitano Halmashauri ya mji Kibaha imeweza kupata mafanikio makubwa kwa kujenga shule mpya 11 za msingi pamoja na ujenzi wa shule zipatazo tisa za sekondari ambazo zimeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha sekta ya elimu kwa wanafunzi.

 

Naye Diwani wa Kata ya Maili moja Mhe.Ramadhani Lutambi ameweza kubainisha kuwa katika eneo la sekta ya elimu kiwango cha ufaulu kimeweza kuongezeka kwa kiwango kikubwa kutokana na kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha miundombinu rafiki kwa wanafunzi ikiwemo kutenga milioni 400 kwa ajili ya kusambaza madawati katika shule mbali mbali ili kuwawekea mazingira mazuri ya manafunzi kuongeza kasi ya ufaulu.


Nao baadhi ya madiwani hawakusita kumpongeza kwa dhati Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kibaha mji kwa juhudi zake za kuweza kupambana kuongeza kasi ya makusanyo ya mapato ya nadani amabyo yameweza kuleta matokeo chanya katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.


Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kibaha mjini Dkt. Rogers Shemwelekwa amempongeza Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hasan kwa kuweza kutenga fedha nyingi ambazo zimeweza kuleeta matokeo chanya katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwa kipindi cha maika mitano.


Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka amesema kwamba maendeleo ambayo yampatikana ni kutokana na fedha nyingi ambazo zimeletwa na Rais Samia ambazo kwa kiais kikubwa zimeweza kufanikisha miradi mbali mbali ikiwemo juhudi za mkurugenzi kukusanya mapato ya ndani ambayo nayo yameweza kusaidia katika miradi mbali mbali.


Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mwalimu Mwajuma Nyamka hakusita kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameweza kuthubutu kutenga fedha kwa maslahi ya wananchi sambaamba na kuwaponegeza madiwani wote pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka ambao kwa pamoja wameweza kushirikiana bega kwa bega katika kuleta maendeleo na kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo.


Halmashauri ya Kibaha mjini kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka wa 2020 hadi 2025 imeweza kutekeleza kwa kiasi kikubwa miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya,, maji, elimu, miundombinu ya barabara, fursa za kutoa mikopo kupitia mapato yake ya ndani pamoja na fedha kutoka serikali kuu ambazo zinatolewa na Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi maendeleo.


                                      


Post a Comment

0 Comments