Shule yetu ya Sekondari The Lord's Hill ipo katika mazingira tulivu na safi ya Ilula, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa. Tumejenga mazingira bora ya kujifunza na kuishi, ambapo wanafunzi wanapata nafasi ya kusoma kwa utulivu na amani, huku wakifundishwa maadili mema na msingi wa kiroho.
Tunaamini kwa dhati kuwa kila mtoto ana uwezo wa kufaulu. Kauli mbiu yetu ni: "Hakuna mwanafunzi aliyezaliwa kufeli." kwetu sisi mwanafunzi yeyote hupokelewa kwa upendo,hufundishwa kwa bidii, na husaidiwa mpaka kufikia ndoto yake. Tuna walimu wenye upendo, uzoefu, na dhamira ya kweli ya kumjenga mwanafunzi kielimu na kimaadili.
Shuleni kwetu The Lord'sHill, tunamfundisha mtoto ajitambue, awe na heshima kwa wengine, na zaidi ya yote, awe na hofu ya Mungu. Tunaamini kuwa mafanikio ya kweli hujengwa juu ya misingi ya maadili mema na kumcha Mungu. Hii ndiyo sababu tunamlea kila mwanafunzi kwa kuzingatia mafunzo ya kiroho sambamba na taaluma.
Mazingira ya shule ni rafiki kwa mwanafunzi wa kila ngazi. Tuna mabweni ya kisasa, chakula bora, usalama wa kutosha, na huduma za kiafya ndani ya shule. Vilevile, tunatumia mbinu za kisasa za ufundishaji, zikiwemo TEHAMA na mafunzo kwa vitendo ili kuhakikisha wanafunzi wetu wanakuwa na uelewa mpana na ujuzi wa maisha.
Karibu sana shule ya Sekondari The Lord'sHill, mahali ambapo ndoto za mwanao hupewa nafasi ya kuota, kukua, na kuzaa matunda. Tunatarajia kuwa na Usaili wa kidato cha kwanza 2026 mnamo tarehe 20/09/2025. Pia mafunzo ya awali ya kidato cha kwanza( PRE-FORM ONE) yataanza tarehe 22/09/2025.
WEKEZA ELIMU BORA KWA MWANAO NA THE LORD'S HILL SEKONDARI, KIWANDA CHA WATAALAMU.
PIGA SIMU NAMBA +255 766 622 908
Mkuu wa Shule.







0 Comments