Na Magrethy Katengu--Dar es salaam
MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour Party(TLP) ,Richard Lyimo amejitosa kuwania nafasi ya Ubunge Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025 Jimbo la Vunjo Mkoani Kilimanjaro .
Amebainisha hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari Katika mahojiano maalumu Agosti 1, 2025 Makao Makuu ya cha hiko ,Magomeni Jijini Dar es Salaam,ambapo amethibitisha kuwania nafasi hiyo na anatarajia kwenda kuchukua fomu hivi karibuni Katika Ofisi zilizopo Vunjo.
"Nimeamua kuwania nafasi ya Ubunge ili niweze kwenda kuwatumikia Wananchi wangu pamoja na kutatua Changamoto zinazowakabili wakazi wa eneo hilo",Amesema Lyimo
Pia,amesema mara baada ya kuchukua fomu ya Chama kuanzia tarehe 14 atakwenda kuchukua fomu za Serikali kwa ajili ya kujaza na kurudisha fomu hiyo ili kutetea nafasi yangu katika Chama Changu.
Aidha,ametoa wito kwa wagombea kuepukana na Rushwa kwa ajili ya kupigiwa Kura kwani rushwa ni adui wa haki,hivyo Mimi naenda kuwapambania Wananchi wa Vunjo na watarajia kuwawakilisha vema endapo watanipa Rushwa kwa nafasi hiyo.
Hata hivyo ,ameeleza kwamba kwa Mwaka huu Chama chetu tunajivunia kuwa na wagombea wengi waliojitokeza kuwania nafasi za Ubunge na Udiwani kwa hiyo tunaamini kupata nafasi za kutosha za kuwaletea wananchi.
"Kwa mara ya Kwanza TLP tunaowagombea wengi kuliko miaka ya iliyopita na tunawataka wale watakaopitishwa na Chama kufanya kampeni za kistaarabu ambazo hazitavunja Maadili ya Uchaguzi,tufanye chaguzi zenye Maadili ili kuendeza historia ya Nchi yetu kwamba ni Kisiwa cha Amani",Amesema Mwenyekiti
Sambamba na hayo, amewataka Wananchi wasichague Viongozi kwa kufuata mihemko ya siasa bali wazingatie Viongozi watakao waletea maendeleo na watakaokwenda kuwawakilisha vizuri Bungeni.
Aidha, ameeleza Katika mchakato mzima wa uchukuaji wa fomu wamejitokeza Vijana wengine na wanawake hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam karibia majimbo yote yamepata wawakilishi wanawake.


0 Comments