Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mshauri na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Ubungo, Samina Patrick, amempongeza Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta mbalimbali nchini, hususan katika Wilaya ya Ubungo.
Samina alisema Rais Samia amekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo kupitia miradi mbalimbali inayolenga kuboresha maisha ya wananchi.
Alisema uwekezaji mkubwa umefanyika katika Wilaya ya Ubungo kupitia miradi ya maendeleo na shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi ambazo zimechangia kukuza maendeleo ya eneo hilo.
Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza katika kongamano la wanawake wa Wilaya ya Ubungo lililofanyika tarehe 7 Machi 2026 katika eneo la East Africa Commercial and Logistics Centre (EACLC) lililopo Ubungo jijini Dar es Salaam.
Samina alisisitiza kuwa wanawake wa Wilaya ya Ubungo wanaendelea kumuunga mkono Rais Samia kwa kutambua juhudi zake za kuleta maendeleo na ustawi wa wananchi.
Aliongeza kuwa wanawake wana mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa na wanapaswa kuendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ili kuijenga jamii yenye ustawi.
Aidha, aliwataka wanawake kuendelea kushirikiana na serikali katika juhudi za kuleta maendeleo na kuimarisha ustawi wa jamii kwa ujumla.
Vilivile mgeni Rasmi katika Kongamano hilo la ubungo alikuwa Mwenyekiti wa uwt Taifa ,Comrade Marry Chatanda ambapo alisema kwamba
Alisema dunia ilitambua kuwa usawa wa kijinsia si anasa bali ni msingi muhimu wa maendeleo ya jamii. Alikumbusha kuwa katika historia ya kimataifa, mkutano wa wanawake uliofanyika Beijing mwaka 1995 uliweka msingi wa wanawake kudai haki zao katika vyombo vya maamuzi.
Chatanda alieleza kuwa hatua kubwa imepatikana nchini Tanzania baada ya nchi kuwa na Rais mwanamke, Samia Suluhu Hassan, aliyeshinda uchaguzi kwa asilimia 97.6 ya kura.
Alisema takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 34 ya nafasi za uteuzi serikalini zimechukuliwa na wanawake, hali ambayo ni ishara ya mageuzi makubwa katika jamii.
Akitoa mfano wa kauli ya Nelson Mandela, Chatanda alisema kumpa mwanamke nafasi ni kuwekeza katika mustakabali wa taifa.
Aidha, alisema Rais Samia aliahidi kutenga zaidi ya shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kiuchumi, huku pia katika sekta ya manunuzi kupitia Public Procurement Regulatory Authority vikundi vya wanawake vikitengewa asilimia 30 ya fursa za zabuni.



0 Comments