Hayo Aliyasema Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mhandisi Zena Said, hapo jana tarehe 1/8/2025 katika Uzinduzi wa jukwaa la kwanza la wahitimu wa Taasisi ya Uongozi(Uongozi institute)ambapo alisema kuwa
"Hiki ni chuo ambacho kinalenga kuleta mabadiliko ndani ya Afrika na nje Afrika"
“Kinachonivutia zaidi kuhusu wahitimu wa Taasisi ya UONGOZI ni utofauti wao. Utofauti huu unaongeza thamani kwa kutoa mitazamo mipya, kuvunja dhana potofu na kuleta fursa mpya za ukuaji na ubunifu,” alisema.
Aliongezea kwa kusema kuwa" Miongoni mwa faida za utofauti huo zilizobainishwa ni pamoja na na Mtazamo wa kimataifa, Uelewa wa tofauti za kitamaduni katika biashara, Kuthamini mitindo tofauti ya uongozi, Mageuzi ya binafsi, Mageuzi ya kitaaluma, na Kufikiri kwa ubunifu" alisema Eng Zena Said
Vilevile Mhandisi Zena aliwapongeza wahitimu wa taasisi hiyo kwa mafanikio yao binafsi na kuwahimiza kuendeleza maadili ya uongozi wa mabadiliko kwa faida ya jamii, mashirika yao na taifa kwa ujumla"
"Wengine mmeingia kwenye nafasi za uteuzi,ambapo naamini mkipewa majukumu mtaweza kuyafanya vizuri hivyo Yoyote kati yenu akipewa fursa ya uongozi katika ngazi Fulani naamini ataweza"
"Unganisha version yako ya masomo na version ya nchi,na mkifanya hivyo mtasaidia watu wengine kuwaleta watu wengine hapa ili kujiendeleza"
Na aliongezea kwa kusema kwamba"Tulizindua Dira yetu ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050,na wananchi wanajua wanatekelezaje Dira!!!
"Serikalini tuko wachache wananchi wapo wengi,hivyo mwananchi mmoja mmoja anatakiwa ajue wajibu wake nini ili kutekeleza Dira"
"Lazima tushikilie Dira yetu ili kila mtu aelewe kuwa atafanya nini,mfano serikali itatengeneza miundombinu ya kilimo,lakini wananchi wanatakiwa wakalime"
"Kwa maana hiyo kuna haja ya Dira mnatakiwa muitafsiri kule Chini ili na wanananchi mmoja mmoja ajue namna ya kutekeleza Dira ya 2050,ili tuweze kukuza uchumi wa nchi na kipato kile tulichojiwekeaIfikapo 2050" alisema Mhandishi Zena Said.









0 Comments