DKT. TULIA ASHIRIKI KIKAO CHA BARAZA LA BAJETI JIJI LA MBEYA.






Leo February 26, 2026. Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge Jimbo la Uyole Mh. Dkt. Tulia Ackson ameshiriki kikao cha baraza la bajeti 2026-2027 kilichoongozwa na mwenyekiti wake ambaye ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Mhe. DorMohamed Issa, kikao kilichofanyika katika ofisi za halmashauri ya Jiji la Mbeya mkoani Mbeya.

Dkt.Tulia ameipongeza ofisi ya Mstahiki Meya kuwa na ukusanyaji mzuri wa mapato yanayoweza kutimiza kile wananchi wanachokikusudia kutoka serikalini.

Dkt. Tulia amekumbushia nia ya halmashauri ya Jiji la Mbeya pamoja na viongozi wote wa serikali kutenga bajeti ya kuongeza mradi wa kujenga madarasa kwa ajili ya kidato cha tano na sita katika shule za sekondari ambazo zitapendekezwa ili kuweza kupata kipato kutokana na ada za wanafunzi zitakazotolewa katika miradi hiyo ambapo kipato hicho kitaweza kukarabati baadhi ya shule za msingi ambazo miundombinu yao ipo chini na kutatua changamoto za madawati kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaotoa msaada katika sekta ya elimu.

Dkt. Tulia pia ametoa ombi kwa mwenyekiti wa kikao hicho kuhusu soko la Uyole ya Kati lililopo katika kata ya Iganjo ambalo linaenda kuhamishwa kwa lengo la kupisha ujenzi wa barabara hivyo ameomba wafanya biashara wa eneo lile watakapoamishwa wakute miundombinu ipo sawa kwa ajili ya matumizi na sio kufika na kusubiri tena ujenzi ukamilike. 

Lakini pia Dkt. Tulia ameongelea miundombinu ya barabara kutokana na adha ambayo wananchi wanapitia ya barabara kujengwa na muda mfupi baada ya ujenzi huo barabara kuwa na mashimo, hivyo amesisitiza kwa kuwaambia watumishi wa TARURA kuhakikisha mkandarasi anatengeneza barabara hizo kwa viwango hitajika ili kutatua changamoto hiyo kwa wananchi.

 Pamoja na hayo Dkt. Tulia amemaliza kwa kumshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu fedha ziweze kutumika kusaidia wananchi kwa ujenzi wa miradi na ukarabati wa baadhi ya miu

Post a Comment

0 Comments