BENKI YA AZANIA YAZINDUA HUDUMA MUHIMU KUWANUFAISHA WANAVYUO NA WAFANYAKAZI


KATIKA kuendeleza juhudi za Serikali za kuboresha sekta ya Elimu na kutoa unafuu kwa wafanyakazi,Benki ya Azania imezindua huduma mbili mpya ambayo "Boom Advance" zitakazonufaisha wanafunzi wa elimu ya juu  na  "Salary Advance" kwa wafanyakazi serikalini na wa sekta binafsi wenye mkataba na Benk ya Azania.

Akizungumza katika uzinduzi huo mbele ya Waandishi wa habari,Ofisa Mwandamizi wa Idara ya Masoko,Bi Elizabeth Nyattega,amesema Boom Advance inawalenga Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wanaopata mikopo kupitia Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu(HESLB).

"Kupitia huduma hii,wanavyuo hawatalazimika kusubiri hadi mikopo yao iingie kwenye akaunti,bali wataweza kupata mkopo wa muda wenye masharti nafuu ili kujikimu wakati wakisubiri fedha kutoka HESLB"Amesema 

Kuhusu,Salary Advance ,Bi Nyattega,amesema  huduma hiyo itawawezesha mwajiriwa kupata sehemu ya mshahara wake kabla ya tarehe ya kawaida ya kuingizwa kwa mshahara.

"Kupitia mkopo huu muda mfupi mwajiriwa ataweza kukidhi mahitaji yake muhimu ya kifedha wakati akisubiri mshahara kuingia mwisho wa mwezi.Mkopo hutarudishwa mara moja mshahara unapowasili,kwa riba nafuu ya asilimia tano na mteja anaweza kukopa hadi nusu ya mshahara wake wa mwezi"amesema Nyattega na kuongeza kuwa mteja anaruhusiwa kukupa kiasi cha mpaka asilimia 50 ya Boom au mshahara na tayari Benki imeanza kutoa mikopo hiyo.

Kadhalika ,Ofisa huyo amesema huduma hizo zote ninapatikana kwa urahisi kupitia simu ya mkononi kwa kubofya *150*75# kupitia Azania Bank Mobile App au Internet Banking.

"Benk ya Azania imeendelea kufanya maboresho makubwa katika huduma zake kiasi cha kutunukiwa Tuzo ya Ubora Kidigitali Afrika Mashariki 2025 katika Tuzo za Africa Bank 4.0 Award 2025 zilizotolewa na taasisi ya Kimataifa ya BII finance mwaka huu"Amesema

Post a Comment

0 Comments