KAMPUNI YA KITANZANIA YASHINDA TUZO YA KIMATAIFA YA LOGISTICS AFRIKA

 



Kampuni ya Kitanzania ya usafirishaji wa mizigo, Xerin Group Limited, imeibuka mshindi katika tuzo za Shining Stars Africa Awards, ikiwa miongoni mwa kampuni zinazoongoza kwa ubunifu na mchango katika sekta ya logistics na air cargo barani Afrika.

Akizungumza kufuatia ushindi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Hussein Jamal, alisema tuzo hiyo ni uthibitisho wa jitihada za kampuni katika kuboresha mifumo ya usafirishaji wa mizigo na kuunganisha biashara kati ya Afrika na dunia.

Alieleza kuwa ushindi huo si wa kampuni pekee bali ni fahari kwa Tanzania, akibainisha kuwa sekta ya logistics ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi kwa kuwezesha biashara kuvuka mipaka ya kitaifa.

Xerin Group Limited imekuwa ikitoa huduma za usafirishaji wa mizigo kwa njia ya anga, bahari na nchi kavu, ikiwa na operesheni zake nchini Tanzania na Dubai, hatua inayorahisisha usafirishaji wa bidhaa kati ya Afrika na masoko ya kimataifa.

Aidha, Jamal alisisitiza kuwa kampuni

Post a Comment

0 Comments