wa vijana kudumisha amani na kuwa wazalendo umetolewa Machi 23, 2026 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Urithi wa Utamaduni na Maadili ya Taifa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Julieth Kabyemela, wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa maadhimisho ya Siku ya Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika uliofanyika katika Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Kabyemela alisisitiza umuhimu wa kutoa elimu kwa vijana kuhusu historia ya taifa lao ili waweze kutambua thamani ya uhuru na kuendeleza uzalendo. Alieleza kuwa Tanzania ina urithi wa kipekee wenye thamani kubwa ukilinganisha na nchi nyingi barani Afrika.
Aidha, alifafanua kuwa maadhimisho ya Siku ya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika yanayofanyika kila mwaka Machi 23 chini ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yana mchango mkubwa katika kuimarisha uelewa wa historia ya ukombozi.
Kwa upande wake, Mratibu wa Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika, Bw. Christopher Mhongole, alisema kuwa kituo hicho kimeandaa matukio mbalimbali yakiwemo maonyesho ya kihistoria na mijadala inayowaleta pamoja wadau kujadili masuala ya ukombozi wa Afrika.
Alibainisha kuwa lengo la matukio hayo ni kuelimisha jamii kuhusu historia yao, kutambua urithi uliopo nchini, na kuhamasisha juhudi za kulinda na kuhifadhi urithi huo.
Bw. Mhongole aliongeza kuwa kupitia historia ya ukombozi, vijana wanapata fursa ya kujifunza uzalendo kutoka kwa viongozi wa zamani na hivyo kuhamasika kuendeleza juhudi hizo kwa maendeleo ya taifa.
Pia alieleza kuwa kituo hicho kilianzishwa mwaka 2011 kwa azimio la Umoja wa Afrika, kikiwa na jukumu la kuratibu na kuhifadhi historia ya ukombozi pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za Afrika.
Kwa mchango wake, alisema Tanzania imepewa heshima ya kuwa kitovu cha taarifa muhimu za kihistoria kuhusu ukombozi wa bara la Afrika, hali inayofanya nchi kutambuliwa kimataifa kama sehemu muhimu ya kumbukumbu za historia hiyo.
Kwa ujumla, vijana wa Tanzania wamehimizwa kuendelea kulinda amani na kuimarisha uzalendo ili kuenzi mchango wa viongozi waliopigania uhuru wa bara la Afrika.

0 Comments