CCM KIBAHA MJI YAUNGANA NA OFISI YA RITA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA KWA WANANCHI



NA VICTOR MASANGU,KIBAHA

Uongozi wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji imeamua kushirikiana na ofisi ya vizazi na vifo kwa lengo la kuweza kutatua changamoto ya ukosefu wa vyeti vya kuzaliwa.

Zoezi hilo ambalo limefanyika katika kata ya Visiga limeedeshwa na wataalamu mbali mbali kutoka Ofisi ya vizazi na vifo kutoka Manispaa ya Kibaha Mkoa wa Pwani.

Hatua hiyo ya kuwasaidia wananchi wa kata ya Visiga imekuja ikiwa ni ziara ya kikazi ya Mwenyekiti CCM Mwalimu Mwajuma Nyamka kwa lemgo la kutoa shukrani kwa wanachama na wananchi kukipa kura nyingi za kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyeki wa CCM Wilaya ya Kibaha mjini Mwajuma Nyamka amesema wameamua kushirikiana bega bega na Rita kutokana na kuona kuna uhitaji wa wananchi wengi kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa.

"Nipo katika ziara kata ya Visiga yenye lengo la kuwashukuru wanachama wa ccm pamoja na wananchi kwa ujumla pia tumeshirikiana na Ofisi ya Rita ili kuwasaidia wananchi kupata vyeti vya kuzaliwa,"amebainisha Nyamka.

Aidha Nyamka amewaomba wanachama wa ccm kuungana kwa pamoja na kuleta chachu ya maendeleo kwani uchaguzi tayari umemalizika hivyo ni jambo la msingi kuwa kitu kimoja na kukijenga chama.

Nao baahi ya wananchi wa Kata ya visiga wamepongeza juhudi ambazo zimefanywa na Mwenyekiti wa CCM kwa kuweza kuwasogezea huduma hiyo kwa ukaribu zaidi.

Pia wamesema wanannchi wengi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto hiyo ya kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa hivyo hatua hiyo itakuwa ni mkombozi mkubwa katika kupata vyeti hivyo.

Ziara ya Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) leo imefikia siku yake ya pili katika kata ya Visiga ambapo imeweza kutoa fursa kwa wananchi kupata huduma kutoka Ofisi ya vizazi na vifo (Rita).



       MWISHO

Post a Comment

0 Comments