Mh.Ridhiwani Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 9 ya UONGOZI Institute yatakayofanyika Mei 15, 2026 jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya taasisi hiyo, Ridhiwani Kikwete ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, atahudhuria hafla hiyo jijini Dar es salaam,huku akitarajiwa kuzungumza na wahitimu pamoja na wageni mbalimbali watakaoshiriki katika mahafali hayo.
Mahafali hayo yanawakutanisha washiriki wa programu mbalimbali za maendeleo ya uongozi zinazoratibiwa na UONGOZI Institute kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi.
Aidha, taasisi hiyo imeendelea kusisitiza dhamira yake ya kuendeleza uongozi bora na maendeleo endelevu kupitia mafunzo na programu za kuwawezesha viongozi katika sekta mbalimbali barani Afrika..
Katika tukio hilo, wahitimu wanatarajiwa kutunukiwa vyeti baada ya kukamilisha mafunzo yao katika nyanja za uongozi, utawala na maendeleo ya jamii.



0 Comments