Na Victor Masangu,
Serikali ya awamu ya sita imeandaa maboresho ya kisera na kisheria yatakayowaondolea changamoto kwa vijana wajasiriamali vikwazo vya muda mrefu vya ukosefu wa dhamana za mikopo katika kuimarisha mifumo ya udhamini wa mikopo ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa katika kutimiza ndoto zao.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla ya fainali ya shindano la Vijana uchumi Challenge kwa mwaka 2026 ambalo limeambana na utoaji wa tuzo kwa washindi.
Katika kilele cha hafla hiyo ambayo imefanyika katika ukumbi wa kituo cha kimataifa Julias Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam na kuhudhuri na viongozi mbalj mbali wa serikali pamoja na viongozi wa dini.
Dkt.Mwigugulu amesema kwamba changamoto kubwa anbazo zinazowakabili vijana wajasiriamali sio ukosefu wa mitaji pekee bali ni ukosefu wa dhamana ambazo zinazokubalika na taasisi za fedha ili kuwawezesha kupata mikopo kwa ajili ya kuendelea shughuli za uzalishaji.
Pia Waziri mkuu ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha kwamba wanaweka misingi imara ya kuwalea vijana mbali mbali wenye mawazo bunifu ambayo yataisaidia serikali katika nyanja mbali mbali.
Kadhalika amewaasa vijana hao kutumia fursa mbali mbali zilizopo ambazo zinatolewa na serikali na kuachana kabisa na tabia ya kutumia vibaya mikopo wanayopatiwa ikiiwemo kugawana.
Kwa upende wake Waziri wa nchi Ofisi ya ya Rais maendeleo ya vijana Dkt.Joel Nanauka amesema kuwa serikali itaendelea kuwaunganisha vijana ambao wana mawazo bunifu na mifumo ya uwezeshaji ili kuyawezesha mawazo hayo kukua na kuweza kuwa biashara zenye kuleta tija.
Dkt.Nanauka amesema kwamba jumla ya mawazo bunifu yapatayo 7862 kutoka Tanzania bara na Zanzibar yaliwasilishwa katika shindano hilo baada ya hatua ya kufanyika kwa mchujo na uchambuzi kwa washiriki 100 waliweza kuchaguliwa na kupatiwa mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo ambayo yalifanyika kwa siku nne katika shule ya uongozi Mwalimu Julias Nyerere Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani.
Naye mshindi wa kwanza katika shindano hilo Jofrey Sanga ambaye amejinyakulia kitita cha kiasi cha shilingi milioni 50 ameipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa kuwashirikisha vjjana kutoa mawazo bunifu ambayo yatawasaidia serikali katika nyanja mbali mbali.
Katika fsinali za shindano hilo la Vijana uchumi Challenge kwa mwanza 2026 mshindi wa kwanza amekabidhiwa hundi ya kiasi cha shilingi milioni 50,mshindi wa pili milioni 30 uku mshindi wa pili milioni 20.



0 Comments