CWT MKOA WA PWANI YASHUSHA NEEMA YA MATOFALI ELFU MOJA SHULE YA MSINGI MKOANI

 


Na Victor Masangu,Pwani 

Chama cha walimu (CWT) Mkoa wa Pwani katika kushirikiana na serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya elimu imeamua kuchangia matofali elfu moja katika shule ya msingi Mkoani iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.


Akikabidhi matofali hayo kwa niaba ya viongozi wenzake Katibu wa CWT Mkoa wa Pwani Suzan Shesha katika halfa fupi ambayo imefanyika katika viwanja vya shule hiyo na kuhudhuliwa na viongozi wa CWT ngazi ya Wilaya na Mkoa pamoja na walimu.


Akizungumza mara baada ya kukabidhi matofali hayo katibu huyo amebsinisha kwamba lengo kubwa la kutoa msada huo ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya elimu.


"Leo tumekuja katika shule hii ya msingi Mkoani na kitu kikubwa tumekuja kutekeleza ahadi yetu ya kukabidhi matofali elfu moja ambayo tuliyaahidi kuyatoa katika harambee na kwamba ni kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa shule,"amebainisha Katibu Suzan.


Aidha amebainisha kwamba wao kama CWT wamekuwa mstari wa mbele katika kuungana na jami katika suala zima la kuleta chachu ya kimaendeleo katika elimu na mambo mbali mbali.


Naye Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Pwani Hamdani Kisoma akitoa salama za chama amesema kuwa malengo yao makubwa ni kuendelea kusapoti sekta ya elimu katika maeneo mbali mbali.


Ameongeza kuwa msaada huo wameutoa ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya mwalimu duniani ambayo ufanyika kila mwaka mwezi octoba hivyo wameona kutumia fursa hiyo ya kutoa sapoti na msada katika shule hiyo.


Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mkoani Adelhelma Shawa ameupongeza uongozi mzima wa UWT Mkoa wa Pwani na Wilaya kwa kuona umuhimu wa kwenda kuchangia msaada wa matofali elfu moja kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa uzio.


"Shule hii ya mkoani ambayo ipo katika mchepua wa masomo ya kiingereza inakabiliwa na changamoto mbali mbali mbali ikiwemo suala la uzio kwa hiyo nawapongeza kwa dhati CWT Mkoa na Wilaya kwa kutushika mkono wa sapoti ya matofali elfu moja,"amebainisha Mwalimu.


Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Mkoani B Salimu Kisaka akusita kutoa shukrani za kipekee kwa CWT kwa kuweza kutoa msaada huo ambao utasaidia katika kuendelea na ujenzi wa uzio huo.


Post a Comment

0 Comments