KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA AKOSHWA NA MRADI WA UZALISHAJI WA MICHE IHOMBE


Na mwandishi wetu, Mbeya 

Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 umetembelea na kukagua mradi wa Kikundi cha Vijana ambao wanaotesha Miche, ambao upo katika Kijiji cha Ihombe, Kata ya Utengule Usongwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, kinachojishughulisha na uoteshaji wa miche ya parachichi na kahawa. 

Mradi huo umetokana na fedha za mkopo wa asilimia kumi ambapo wameweza kupatiwa Shilingi milioni 30 kutoka Halmashauri katika mwaka wa fedha wa 2025/2026.

Katika kikundi hicho kimeweza kufanikiwa kuongeza vitalu vitatu na kufikisha jumla ya vitalu vitano huku mtaji wake ukifikia Shilingi milioni 33 kutoka mtaji wa Shilingi milioni tatu (3) waliokuwa nao awali.

 

Mradi huu umewezesha uzalishaji wa miche 80,000 ya parachichi hadi sasa, huku Shilingi milioni 33 zikitumika katika ununuzi wa pembejeo ikiwemo samadi, udongo, viriba pamoja na gharama za vibarua.


Mradi huu umewezesha vijana watano kujiajiri na kutoa ajira za muda mfupi kwa zaidi ya watu 200. Kikundi kimetoa miche 20,000 ya miti pori kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa ajili ya upandaji katika hifadhi za milima eneo la Ihombe. 


Hadi sasa, kikundi kimerejesha Shilingi milioni 9.806 katika mkopo wake wenye mkataba wa marejesho ya miaka miwili kuanzia Mei 2026 hadi Aprili 2028.

Post a Comment

0 Comments