BOEING 787-8 DREAMLINER KUPOKELEWA ZANZIBAR

 

Na  Mwandishi  wetu

Serikali inatarajia kupokea ndege Mpya aina Boeing B787-8 Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 262, Ndege hiyo inatarajiwa kupokelewa tarehe 19 .8.2024 katika kiwanja wa Ndege wa Kimataifa cha Abeid Amani Karume .


Akiongea na Waandishi habari Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema  mapokezi ya ndege hiyo yataongezwa na Dkt Hussein Mwinyi Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.


“ Ujio wa  ndege hii ya kisasa yenye masafa marefu aina ya B787-8 Dreamliner kuwezesha ATCL kuongeza miruko ya safari zake kwa  vituo vya Kikanda na Kimataifa ambavyo wanahudumia kwa sasa kwa pamoja” alisema Mbarawa.


Mbarawa amesema kuwa serikali itaendelea kununua ndege na Mwakani mwaka 2025  katikati inatarajia kupokea ndege nyingine mpya.


Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Zanzibar  Dkt. Khalid Mohamed Salum amesema kuwa Serikali ya  Mapinduzi ya Zanzibar inampango wa kununua ndege lakini  kwa sasa inaendelea kuboresha miundombinu ya uwanja wa ndege cha kimataifa cha cha Abeid Amani Karume pamoja na kiwanja cha ndege cha Pemba.


Naye Mwanasheria wa Shirika la Ndege ATCL  John Zunda amesema kuwa kwa sasa ndege haziwezi kukamatwa kwakua Serikali imeshalipa Madeni

Post a Comment

0 Comments