Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam Gamuhamgire amesema kuamempokea katika ofisi zao na tayari amekiwa mwanachama wao na kuwa hatakuwa ni miongoni mwa wachapalazi watakao sukuma gurudumu la mafanikio.
"Kwa sasa nirasmi ataanza kutekeleza majukumu ya uanachama wake ndani ya TADWU nakuwa hali hiyo itaongeza mshikamano,"amesema Gamuhamgire.
Hata hivyo kukaribishwa Msangi anatoka kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Malori Tanzania (CHAWAMATA) huku akiwa na uzoefu wa uongozi wakupambania wafanya kazi wa Malori pamoja na haki mbali mbali za waajili.
Mara baada ya kukaribishwa katika Ofisi hizo Msangi amesema kuwa yapo malengo mengi ya kupambania kero mbali mbali ambapo amelenga kuangazia maeneo yenye kero zenye muda mrefu.
Ametaja maeneo hayo kiwa ni foleni ya Tunduma ,foleni ya Kasumbalesa , foleni ya kushusha na kupakia Lubumbashi katika nchi ya Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo pamoja na maeneo ya Overstay nchini humo.
"Tunakwenda kupambania mambo mengi katika kujenga taswira mpya ya kushugulikia utatuzi was kero zinazoonekana kuwa za muda mrefu," amesema Msangi huku akidokeza madhingira ya utatuzi katika maeneo hayo akisema kuwa tayari Katibu wa Wizara ya Kazi Ajira na Watu Wenyeulemavu nchini amezingumzia kuambatana katika safari za utatuzi huo.

0 Comments