Mwapwele :TCCIA Kilimo chenyetija Kitarahisisha Masoko

 




Na Francisco Peter

Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wafanya biashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA)Nebart Mwapwele amesema kuwa mipango ya utekelezaji wa kilomo chenye tija nchini itarahisisha masoko mbali mbili.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam  na Mwapwele wakati akipambanua juhudi za kukuza kilimo zinazofanywa na serikali kuhakikisha bidhaa za kilimo hususani  viungo vya Tanzania ambapo vimekuwa vikitambulika  kirahisi katika masoko mbalimbali ulimwenguni ikiwa ni hatua kubwa na muhimu sana katika kukuza mazao na bidhaa za mazao ya viungo nchini.

"Takwimu zinaonesha kwa sasa tunazalisha aina kama 30 ya viungo na kuendeleza aina tano za viungo vya chakula ambavyo ni Karafuu, Mdalasini, Pilipili Manga, Iliki na Tangawizi," Amesema Mwapwele.

Amesema Nembo ya Viungo Tanzania (Tanzania Spices Label) ambayo itarahisisha na kuhakikisha bidhaa za viungo vya Tanzania zinatambulika kirahisi katika masoko mbalimbali ulimwenguni ikiwa ni hatua kubwa na muhimu sana katika kukuza mazao na bidhaa za mazao ya viungo nchini.

 Aidha, Mkurugenzi huyo ameeleaza kuwa uanzishwaji wa Nembo ya viungo Tanzania imekuwa ikichochea kutangaza bidhaa za viungo katika masoko mbalimbali .

Mwapwele ametoa wito kwa Watanzania na kuziomba kampuni kuwekeza kwa kujenga viwanda vya kuongezea thamani mazao yetu ya viungo ili kuongeza tija na kipato kwa wakulima wetu na taifa kwa ujumla.

Mwapwele ameeleza kuwa katika ulimwengu wa masoko ya bidhaa kwa sasa watumiaji wanapenda kutumia bidhaa wanayoiamini na kuifahamu hivyo kama nchi ili tuweze kufanya vizuri masoko yetu yameendelea  kuaminika kwani mazao ya ardhi yetu yanapendwa.

"Kilimo chetu kinalimwa katika ardhi ambayo aina kemikali yoyote kwani bado ardhi yetu katika maeneo mengi haijatumika ,"amesema Mwapwele.

“Brand” katika masoko ya ndani Pamoja na nje ya nchi, ili kuweza kutangaza bidhaa na huduma mbalimbali sokoni rajamu ni suala muhimu sana hata hivyo rajamu ya bidhaa haiishii tu kutangaza bidhaa bali pia kutangaza nchi.

Post a Comment

0 Comments