MWENYEKITI UWT KIBAHA MJINI AKEMEA MAKUNDI NDANI YA CHAMA


Mwenyekiti wa umoja wa wanawake (UWT) Elina Mgonja 


Na Victor Masangu,Kibaha


Mwenyekiti wa umoja wa wanawake (UWT) Elina Mgonja amekemea vikali kuwa na makundi na  tabia ya baadhi ya wanachama  kuwa  wachonganishi na badala yake wahakikishe wanaungana kukiimarisha chama na  ili kiweze kushinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa.


Mgonja ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika kata mbili za Viziwaziwa pamoja na kata ya Kibaha yenye lengo la kuwatembelea wanachama na kuzungumza nao ili kubaini changamoto zinazowakabili ikiwemo kujua uhai wa chama.


Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kwa sasa chaguzi zilishamalizika kwa hivyo hakuna aja ya kuwa na makundi na badala yake wanawake wanapaswa kubadilika na kuhakikisha wanapambana ili kuepukaba na kupoteza nafasi za viongozi katika ngazi mbali mbali.



"Nipo katika ziara yangu ya uwt na nimeongoza na wajumbe ya kamati ya utskezaji sambamba na mlezi wetu mama Selina Koka lkn kitu kikubwa tuachane kabisa na kuwa na tabia ya uwongo nia yetu kubwa ni kushinda,"alisema Mgonja.


Kadhalika alisema kwa sasa anatambua viongozi waliochaguliwa ndio wamepewa dhamana ya kuongoza hivyo inapaswa kuwaheshimu viongozi ambao wapo madarakani ili waweze kutekekeza majukumu yao ipasavyo.


Katika hatua nyingine alitoa pongezi zake kwa mlezi wa UWT Selina Koka kwa juhudi zake za kuwakomboa wanawake katika kujikwamua kiuchumi na kuwasaidia katika mitaji.


                              MWISHO

Post a Comment

0 Comments