RC KUNENGE ATEMBELEA KUKAGUA BARABARA ILIYOHARIBIWA NA MVUA CHALINZE






Mkuu wa Mkoa Pwani Mhe.Abubakar Kunenge Leo April 17.2023 amefika  Kimange -Chalinze kukagua na kujionea ujenzi wa kalavati lililoharibiwa na mvua kubwa zilizonyesha April 15.


Mvua hizo zilipelekea kubomoka kwa kingo za  kalvati Barabara hiyo kuu ya Chalinze Segera na kuathiri watumiaji wa Barabara hiyo.


Mhe Kunenge ameeleza Serikali inaendelea kerejesha hali ya Barabara hiyo katika hali ya kawaida na kazi ya Ujenzi huo inakamilika leo. Amewataka watumiaji wa Barabara kutii maelekezo ya Jeshi la polisi la kutumia upande mmoja wakati wakisubiri zege kukauka.

Post a Comment

0 Comments