WANNE FAMILIA MOJA WAJARIKI WA MOSHI WA JENERETA DAR ES SALAAM




Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza tukio la vifo vya watu wa nne wa

familia moja ambao wamepoteza maisha baada ya kuvuta hewa  chafu ya moshi kutoka kwenye jenereta walilowasha ndani ya nyumba na baadae kulala.


Tukio hilo la  kusikitisha limetokea siku ya tarehe 18. 04. 2023 majira ya saa 4:00 usiku baada ya watu hao kuwasha jenereta mara baada ya umeme kukatika kisha kuliweka ndani ya nyumba.


Uchunguzi wa awali wa Jeshi hilo unaoneshakuwa 

watu hao walipoteza maisha baada ya kuvuta hewa inayodaiwa kuwa ni hewa ya moshi

iliyokuwa inatoka kwenye jenereta baada ya kuwashwa.


Watu waliopoteza maisha ni Kazija Mohamed (21), Munir Ibrahim(7), Munira Ibrahim(6), Muyyat 

Ibrahim (3). Huku Mume na mke  Ibrahim Juma (28) na Aisha Ayubu(29) wote wakazi wa Kilimahewa, Chang’ombe wanapatiwa matibabu ambapo inaelezwa hali zao sio nzuri na wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali 

Taifa ya Muhimbili.

Post a Comment

0 Comments