Teophil Mbunda: (Dar es Salaam)
Serikali imewataka wananchi kupuuza taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ya kuuzwa Kwa Bandari ya Dar es salaam Kwa kuSema kuwa tuhuma hizo ni za uongo Kwan serikali imesaini mkataba wa makubaliano na Dubai ya kuendesha Bandari na si mkataba wa utendaji..
Akitoa ufafanuzi huo Leo Juni 8 jijini Dar es salaam msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa amesema kuwa serikali imesaini mkataba wa ushirikiano ambao mjadala wake utadumu Kwa miezi 12 kabla ya kuingia kwenye mkataba wa utendaji kazi ambapo Bunge limefungua uwanja wa kupokea maoni kutoka Kwa wananchi kuhusu makubaliano hayo.
Amesema ufanisi wa Bandari ni mdogo hivyo unahitajika uwekezaji ili Bandari iweze kujiendesha Kwa faida na kuendeleza Pato la Taifa
"Bandari zote duniani zinaendeshwa Kwa ushirikiano yaani uwekezaji na utendaji wa Bandari unataka uwekezaji ili kuepuka kuingiza deni Kwa taifa tumekopa tilioni 1.2 Kwa ajili ya utanuzi wa Bandari hili tayar ni deni Kwa taifa"amesema Msigwa
Aidha Msigwa amesema kuwa ukifika wakati wa kusain Mikataba utazingatia zaidi maslahi ya Taifa.
Sambamba na hayo Msigwa amewataka waandishi wa habari wa mtandao kufanya kazi Kwa weredi na kuepuka kutumika vibaya katika kupotosha umma
Amesema ili kuendelea kuthamini utendaji kazi wa vyombo vya habari mitandao ofisi yake itaanza kuratibu vyombo hivyo ili viweze kushirikiana na serikali katika kuabarisha umma huku akitoa Rai Kwa ambao wanafanya kazi hiyo bila ya kuwa na taaluma kuanza kusoma ili wawe na sifa
0 Comments