AJINYONGA BAADA YA KUMCHARANGA MAPANGA MKE WAKE SABABU NI KUKUTA SMS ZA MAPENZI.


Geita


Martine John (40) Mkazi wa Geita Mjini amejinyonga hadi kufa baada ya kumjeruhi mke wake kwa kumkata na panga sehemu mbalimbali za mwili wake na kudhani kuwa amefariki huku chanzo cha tukio hilo likitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.


Mama mzazi wa mwanamke aliyejeruhiwa alisema kwamba sio mara ya kwanza kwa wawili hao kugombana na wamekuwa wakipatanishwa mara kadhaa





"Walishawahi kugombana akaja nyumbani Mkwilima nikawa suluhisha wakarudi nyumbani sasa jana ndo napigiwa simu mtoto wako kachomwa kisu na mkwe wako amejinyonga" amesema Anastazia Paul Mama mzazi wa Majeruhi


Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novemba 22/ 2023 katika mtaa wa 14 Kambarage Halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita.


Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Geita ACP Adam Maro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi baada ya mwanaume huyo kukagua simu ya Mke wake.

Post a Comment

0 Comments