"WAKANDARASI WAZEMBE SIKU ZAO ZINAHESABIKA" BASUNGWA





Na  Sheila  Ahmadi


Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amewataka  na  Wakandarasi ambao wamepewa Miradi ya Ujenzi ya barabara kutetekeleza kwa wakati muda waliosaini Mkataba na amuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Tanroad kuwasimamia na kuwakagua mara kwa mara ili lawama.zisiendelee kuiangukia Serikali.


Agizo hilo amelitoa leo Jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara yake katika Mkoa huo  ikiwemo mradi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka kuanzia Posta mpya ya zamani Maktaba na kuunganika Gerezani, Mradi wa barabara ya Segerea ina kuunganika kimara Bonyokwa  pia Mradi wa barabara ya Msongola Ilala na kuunganishwa na Mbande Temeke ambapo Mkandarasi wake tangu akabidhiwe hakuna chochote alichofanya  hadi amepewa adhabu na kupewa mwezi mmoja aanze kazi mara moja.


Aidha  waziri  huyo  alisema  katika ziara alioanza jana ambayo ilihusisha  na kukagua miundombinu ya barabara mkoani  humo  kutokana na mvua za elnino ambazo zimeathiri  makazi ya watu na miundombinu mbalimbali zikiwemo nyumba za wakazi maeneo ya jangwani nakadhalika huku akitoa ufafanuzi kuhusu wakandarasi ambao hawafanyi kazi kwa wakati huku wakazi wakiendelea kutumia njia mbadala ya kutatua kero io.


"Wakandarasi wote wakiwemo wazawa na wale ambao wanatoka nje ya nchi wajitathimini katika utendaji wenu wa kazi mmekuwa mkisaini mikataba mingi huku mkienda kinyume na makubaliano ya mikataba hiyo huku wengine nimepita katika miradi kadhaa na kuona kazi ikiendelea lakini mradi wa msongola  hadi mbande imenishangaza sana hakuna kazi yeyote iliyofanyika hadi tanroad wanaingilia kati kutoa adhabu hivyo bodi ya wahandisi BRT hili jambo wasilifumbie macho kwani linawatia dosari kwa kutoaminika kwa mtu mmoja akiwa analeta propaganda kwenye fedha za serikali"  Amesema  waziri  Bashungwa.


Sanjari  na hayo waziri  bashungwa alipotembelea mradi wa mwendokasi kutoka posta mpya  hakuridhishwa na utendaji kazi wake kwani mradi alisaini miezi mitatu  lakini wamekuja kuanza miezi mitano badae hivyo amemuagiza mkandarasi ambae  amepewa tenda hiyo aweze kufika ofisini kwakwe aeleze kwanini amechelesha mradi huo hivyo amesema pamoja na sababu zake amesema.mradi huo ukamilike 2024 march.


Kwa upande wake  kaimu mtendaji mkuu wa wakala wa barabara Tanzania (Tanroad) Mhandisi  Doroth Mtenga 

Amesema mradi wa BRT  wa mabasi yaendayo kasi ni mradi ambao unaenda kuanza kwenye sehemu mbalimbali zikiwemo bibititi,   gongolamboto, Posta mpya na nyinginezo ambapo itatumia Garama ya shilingi bilioni 231.


Kwa upande wake Mkuu wa mkoa  wa dar  es salaam Albert  Chalamila  amewataka wakazi ambao wamejenga vibanda vya biashara pembezoni mwa biashara ambapo wabomoe mara moja ili kupisha miradi ya barabara hususani kata ya chanika ambapo baadhi ya wakazi wamekataa na kudai fidia na wameshaenda mahakamani kuishitaki serikali 


Katika ziara hiyo Waziri alikuatana na kero za wananchi ikiwemo miundombinu ya segerea kuwa hatarishi kwa wakazi ambapo mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha maafa kwa wakazi hivyo  waziri amewapa pole na kutoa rai kwa viongozi wakiwemo wakuu wa wilaya, wenyeviti na wabunge na kuwapa mkono wa pole na kuwatafutia maeneo mbadala ya kuishi huku wakisubiri mvua zipite

Post a Comment

0 Comments