Na Sheila Ahmadi
Mkuu wa Wilaya ya ilala Mhe. Edward mpogolo ametoa pongezi kwa mashirika ambayo yameweza kuadhimisha maadhimisho kwenye usawa na haki za kibinadamu nchini.
Hayo yamesemwa Jijini. Dar es salaam na Mkuu wa wilaya ya ilala Edward Mpogolo mara baada ya maadhimisho ya kumbukizi ya maafa yaliyowapata baadhi ya Wananchi nchini ambapo amesema kuwa mashirika yote ambayo yamejitokeza kwenye maafa na uokoaji ni jambo muhimu kwa Taifa kwani tunatakiwa kujenga Taifa na kukuza uchumi wa nchi.
Aidha Mpogolo ameongeza kuwa katika maadhimisho haya yanalenga zaidi kumbukizi na kuwapa wale wote wanaojitoa katika harakati za kuwapigania binadamu wengine kwa hali na Mali ikiwemo OSHA, save the children, Red cross, Zima moto na damu salama.
Naye afisa uhusiano kutoka Wakala wa salama na Afya mahala pa kazi OSHA Eleuter Mbilinyi amesema kuwa sisi kama Wakala wa usalama na Afya mahala pa kazi tunashirikiana na wadau wengine katika utoaji wa Elimu ya maafa na kuhakikisha kuwa mazingira ya kazi yanakuwa salama .
Vilevile OSHA tunashiriki katika kuwatengenezea wafanyakazi mazingira Bora na salama na kutambua umuhimu wao katika kujenga uchumi wa nchi , na kufanya kazi kwenye mazingira mazuri,hivyo vifaa na utekelezaji wa ufanyaji wao kuhakikisha una kuwa wenye weredi mkubwa.



0 Comments