Na Mwandishi wetu
Wananchi watatu ambao ni Raia wa Kitanzania. wamefungua kesi Mahakama Kuu Masijala ya Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupinga Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusimamia uchaguzi wa mwaka huu (2024) wa Serikali za Vijiji, Kamati za Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji .
Kutokana na taarifa iliyotolewa na Dkt Ananilea Nkya ambaye ni mmoja wa Wananchi hao amesema mbele ya Mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kuwa Maombi hayo Jumatano wiki hii Agost, 28 Agosti 2024. nakwamba Maombi hayo yalitajwa kwa mara ya kwanza Agost 22,2024.
Dkt Nkya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania JUKATA amewaomba Wananchi kujitokeza kwa wingi Kwa akili ya kusikiliza kesi hiyo ambayo itasikiliwa majira ya saa nane Mchana Mahakama Kuu Masijala ya Kanada ya Dar es salaam.
"Maombi haya (Misc Cause no 19721 ya 2024 mbele ya Jaji Dyansobera) yalipotajwa Mahakamani kwa mara ya kwanza, Jaji Dyansobera aliwapa wanasheria wa Serikali siku saba, kati ya Agosti 22 na 28 2024, kuleta hoja za Serikali mahakamani ili mahakama izisikilize, kupima na kutoa maamuzi kuhusu maombi ya raia kuzuia TAMISEMI kujihusisha na uchaguzi wa Serikali za Vijiji, Kamati za Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji." Amesema Dkt Nkya
"Sisi kama raia tuliopeleka maombi ya kufungua shauri la Kikatiba Mahakama Kuu tunaamini kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi kufika kwa wingi Mahakama Kuu Dar es Salaam siku ya Jumatano, Agosti 28, 2024 maombi ya shauri hilo yatakaposikilizwa, Raia watapata fursa ya kusikiliza hoja za serikali moja kwa moja kutoka kwa wanasheria wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na hoja za raia kupitia kwa Mawakili wetu kupinga TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa Serikali za Vijiji, Kamati za Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji mwaka huu, 2024.
Kwa upande Wake Bob Wangwe ambaye ni miongoni mwa raia hao waliofungua kesi ya Kupinga TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa amesema kuwa wamefungua shauri hilo kwa kuwa wanatambua kwamba raia ndio mamlaka ya nchi kama inavyothibitishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 8(1)(a)
Ibara hii ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kuwa “Wananchi ndiyo msingi wa Mamlaka yote na Serikali itapata Madaraka na Mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii”
Aidha ameongeza kuwa, kifungu cha 10(1)(c) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Namba 2 ya 2014 kinatoa wajibu na mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa Serikali za Vijiji, Kamati za Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji kwa Tume, siyo TAMISEMI.
Bob Wangwe ambaye Mkurugenzi wa JUKATA amesema uchaguzi ukisimamiwa na mamlaka isiyohusika kuna hatari ya uchaguzi huo kutokuwa na unyoofu, huru na haki na athari zake ni pamoja na kusababisha vijiji, mitaa na vitongoji kuongozwa na watu wasiowaadilifu na wasiowajibika kwa raia, hata kufuja michango na kodi za wananchi.
"Msingi wa Kisheria wa Kesi hii. Maombi ya kesi yanahoji kwamba Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kusimamia uchaguzi kunaleta hatari kubwa kwa haki na uwazi wa mchakato wa uchaguzi. Matukio ya awali ya dosari na upendeleo unaoonekana ndani ya Wizara yamezua maswali juu ya uwezo wake wa kusimamia uchaguzi huu bila upendeleo. Amesema
Naye Bubelwa Kaiza ambaye ni moja wa mmoja wa Wananchi hao amesema kuwa hatua hiyo ya kisheria inalenga kulinda haki ya kikatiba ya raia wa Tanzania kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia ambao ni nyoofu, huru na wa haki.
Hata hivyo ameongeza kuwa baada ya kutungwa kwa sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 2024 na kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ibara ya 74(6)(e) majukumu ya kusimamia uchaguzi wa Serikali za Vijiji, Kamati za Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji yako chini ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
"TAMISEMI kutaka kusimia uchaguzi huu ni batili na kinyume cha sheria. Kwa mujibu wa kifungu cha 1 0(1)(c) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, ni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi pekee yenye jukumu la kusimamia uchaguzi wa Serikali za Vijiji, Kamati za Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji.
Kukosekana kwa Viongozi Halali Kwenye Mitaa, Vijiji, na Vitongoji
Tunahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kufuatilia na kusikiliza maombi ya kesi hii mahakamani kwa sababu uchaguzi wa viongozi wa vitongoji, vijiji na mitaa 2024 usipoendeshwa kwa mujibu wa Katiba, sheria na uadilifu raia wataendelea kukabiliwa na changamoto za maendeleo pasipo msukumo wa uongozi kuwajibika kuzishughulikia.

.jpg)
0 Comments