Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi. Zainab Telack ameutaka uongozi wa chuo cha bahari Dar es Salaam (DMI) kuhakikisha wanaendeleza eneo walilopewa na mkoa huo kwa kujenga tawi la chuo hicho.
Bi Taleck amesema hayo ofisini kwake mara baada ya kuzungumza na uongozi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam(DMI) huku ameutaka uongozi wa chuo hicho kueleza mpango wa kutoa mafunzo ya usalama kwa wavuvi mkoani humo.
“Mkoa wa Lindi unawavuvi wengi na asili ya watu wa Lindi ni Uvuvi na Kilimo hivyo ni muhimu kwa chuo chenu kujenga tawi hapa, eneo tumewapa na tupo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kuhakikisha wavuvi wanapata elimu stahiki ili kukuza uchumi wa Mkoa wa Lindi na taifa letu” Alisema Taleck
Kwa Upande wake Mkuu wa chuo cha DMI Dkt.Tumaini Gurumo amesema kuwa lengo la kufika ofisini kwa mkuu wa mkoa huo ni kueleza mpango wa chuo hicho kuanza kujenga kituo cha mafunzo ya usalama katika utafutaji na uchimbaji wa gesi pamoja na kuendelea kutoa elimu ya uvuvi salama .
“Tunaushukuru sana Uongozi wa Mkoa ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa kwa kutupokea mimi na wenzangu pia kwa kutupatia eneo la kujenga tawi la chuo chetu, hivyo tunaendela kukamilisha taratibu mbalimbali za kuanza ujenzi huo” Alisema Dkt. Tumaini.
Aidha viongozi kutoka chuo cha bahari DMI wameweza kuhudhuria wakiwemo Mkuu wa chuo kutoka DMI Dkt. Tumaini Gurumo hivyo DMI tutakuwa mkoani Lindi kwa siku nne tukiendelea kutoa elimu kwa wavuvi na kutembelea shule mbalimbali za mkoa huo.ili kuweza kutoa elimu ya fursa za masomo yanayohusu bahari kwa wanafunzi wa shule za Sekondari ili wajiunge na chuo hicho ambacho makao makuu yake yapo jijini Dar es Salaam.



0 Comments