Na Mwandishi wetu
Maafisa ustawi wa jamii, Maafisa Elimu, Watendaji kata na Mitaa wametakiwa kuisisitiza jamii mara kwa mara juu ya msingi wa maadili na kuwakumbisha wazazi na walezi kuhusu jukumu la malezi ya watoto kuwa ni lao na wanapaswa kuwaeleza watoto uhalisia wa maisha ya Sasa ili kuwajengea uwezo wa kujilinda.
Akizungumza jijini dar es salaam Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya ubungo Bi.Hilda malosha mara baada ya kufungua mafunzo maalumu kwa maafisa hao katika wilaya ubungo yaliyotolewa na Shirika la Usawa wa Kijinsia Tanzania kwa udhamini wa Women Fund ambapo amesema jamii ikikumbiswa mara kwa mara juu ya kujiepusha na vitendo vya ukatili itaaidia kuboresha maadili na kuwajengea watoto uwezo wa kujitambua.
"Amesema kuwa Elimu ya kijamii inapaswa kukumbushwa mara kwa mara katika Jamii, amewataka maafisa hao na kusimamia jukumu hilo na kusisitiza kuhusu agenda ya ukatili katika jamii ili kukomesha swala hilo.
"Tunatakiwa kila mmoja ajue jukumu lake, tukumbushane tukumbushane ilikila mmoja ajue anaeajibu wa kupinga ukatili katika jamii na kutoshiriki katika hilo".
Kutokana na vikao vya wazazi/walezi na wanafunzi shuleni lakini wazazi na walezi wamekuwa hawajitokezi kwa wingi halii hiyo inafifisha kufikisha ujumbe kwa wazazi kuhusu ukatili na ukizingatia kuwa ukatili kwa sehemu kubwa huanzia katika ngazi ya familia.
Aidha kwenye jamii ambayo ina ukatili haiwezi kuendelea kimaendeleo hivyo tunatoa wito kuwa kinyume cha ukatili ni upendo kwahiyo jamii ikaishi kwa upendo hata wakionya waonye kwa upendo"
Sanjari na hayo amewataka maafisa hao kujiepusha na vitendoa vya ukatili katika ofisi zao kwa kutoa majibu ya kashfa,matani yanayovuka mipaka,amewataka kuwa sehemu kubwa ya kuzuia ukatili.
Naye Afisa mratibu wa mafuzo wa (SHIUKITA) Jamaica Kyando amesema Wameamua kutoa mafunzo hayo katika wilaya ya ubungo baada ya kuabaini kiwa kuna ukatili mkubwa katika jamii hivyo wakaona tija ya kutoa mafunzo kwa maafisa ili kwenda kutoa elimu na kupunguza kwa kiasi kikubwa ukatili wa kijinsia.

0 Comments