Na Mwandishi wetu
Kuelekea Wiki ya Azaki (CSO ) Kufanyika September 09 hadi 13 Mwaka huu Jijini Arusha Huku Baadhi ya taasisi zitashiriki zikiwemo ubongo kids, FCS pia matukio mbalimbali yatafanyika kwenye kutoa ujumbe na elimu kwa umma.
Hayo yamesemwa jijini Dar e es salaam na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Christoffel - Blindenmission kutoka (CBM) Nesia Mahenge ambapo Amesema kuwa Wiki ya Azaki mwaka huu inaenda kufanyika kwa mara ya sita mfululizo na imekuwa na mwitiko mkubwa kutoka kwa wadau na wanachi kwa ujumla.
" Kupitia wiki hiyo tunategemea kutoa elimu kwa wananchi hususani kwa makundi ya vijana,wanawake na wenye ulemavu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (FSC) Justice Rutenge amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni voice,vision & value ikilenga kutoa kipaumbele na thamani kwa mawazo ya maoni ya wananchi juu ya Mstakabali wa maslai ya Taifa ikiwemo Dira ya maendeleo ya Taifa.
Aidha Rutenge amesema kuwa Katika wiki ya Azaki wanasisitiza kila mtu ashiriki katika kutengeneza dira ya taifa na kutengeneza thamani ya malengo ya taifa kwa pamoja.
Hivyo Licha ya utofauti wa mawazo ulipo katika jamii ni lazima tufikie malengo ya kuhakikisha tunapata mawazo ya pamoja na kuwa na Dira ya pamoja.
Vilevile ametoa wito kwa watanzania kuweza kushiriki katika wiki ya Azaki ili kujifunza mengi na kushirikiana kwa pamoja katika kuchagiza maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mtendaji kutoka Ubongo kids Mwasi umwe amesema kupitia Taasisi yao wamewafikia Watoto milion 42, hivyo wamekuja kushirikiana na CSO ili kuwafikia wengi zaidi na ni mara yao ya kwanza na wanaamini ni fursa ya kuwafikia watu wengi na kujenga maslai bora ya Taifa kwa pamoja


0 Comments